Google PlusRSS FeedEmail

DR SHEIN AHIMIZA AMANI NA USALAMA ZANZIBAR.

Dr Shein akihutubia wananchi wa Zanzibar,juu ya Amani na Utulivu.

Na; Ali Msuko, Znz.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ally Mohamed Shein amewahimiza wananchi wa Zanzibar kuimarisha amani waliyonayo na kuachana na vitendo vya vurugu vinanvyofanywa nchini humo na baadhi ya makundi ya watu wachache wanaojiita UAMSHO.

Dr Shein aliyasema hayo juzi alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Zanzibar kwenye baraza la Eid el Hajj lililofanyika kwenye ukumbi wa Salama Bwawani Hotel. Dr Shein alieleza "Serikali itaendelea kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kufuata taratibu kama hatua muhimu ya kuimarisha utawala bora nchini. Hata hivyo, suala la kusimamia taratibu na kuona kuwa sheria zetu zinazingatiwa ni la kila mwananchi na sio serikali pekeyake" alisema Dr. Shein

Zaidi ya hayo, Dr. Shein pia aliwasihi wananchi wote juu ya umuhimu wa kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio msingi mkubwa wa amani na utulivu tulionao.
Dr. Shein pia alizungumza juu ya fujo zilizotokea nchini humo kati ya tarehe 17/10 na tarehe 19/10 zilizopelekea kuchomwa moto kwa maskani za CCM, kuvunjwa maduka, kuporwa mali za watu na pia kupelekea kuuliwa kwa askari wa Polisi wa Kikosi cha FFU No. F2105, Koplo Said Abdulrahman. Aliwaasa wananchi kutojihusisha na vitendo vya fujo na vurugu vinavyolenga kuvunja amani. Pia alitoa pole kwa familia ya marehemu na wananchi wote kwa ujumla walioathirika na vurugu hizo.

This entry was posted in

Leave a Reply