Google PlusRSS FeedEmail

WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE WACHUKULIWE HATUA


serikali ya wilaya ya kilwa imewataka wazazi na walezi wanaotakaza
watoto wao kwenda shule wachukuliwe hatua za sheria ili kukomesha
vitendo hivyo.

Agizo hilo limetolewa na  mkuu wa wilaya Kilwa Abdala Ulega wakati
alipokuwa anazungumza  na wazazi walezi na wadau wa elimu wa shule ya
sekondari mibuyuni  wilayani humo jana.
                      Ulega alisema kufanya  hivyo sio  tu kwamba ni kuwa nyanyasa bali  pia
ni kuwanyima  hakiyao ya msingi  na urithi wa maisha yao ya baadaye
watoto ambao ndiyo tegemeo la taifa.

Watendaji wa  tarafa, kata, kijiji wametakiwa  kutekeleza  agizo hilo
kwa kuwachukulia hatua  wazazi na walezi   aina hiyo.

Alisema kuwa  kuwakataza watoto kwenda shule mbali na kuwanyima haki
zao vilivile kunakwamisha juhudi za serikali  za kukuza elimu.

Ulega alitoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuwa zaidi ya watoto
200 wa shule ya sekondari Mibuyuni hawafiki shuleni kutokana na utoro
wa rejareja na kusababisha shule hiyo kuwa  na mahudhurio  madogo kila
siku.

Aidha shule ya sekondari  mibuyuni  ambayo iko katika wilaya Kilwa
Mkoani Lindi ni  kati ya shule 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya
kitado cha nne mwaka huu.

This entry was posted in

2 Responses so far.

  1. abdulaziz says:

    HONGERA SANA DC ULEGA Ila jukumu kubwa ni kuhakikisha Bwege anarudisha Ubunge kwa CCM na Idadi ya madiwani,Mitaa,Vijiji vingi virudi..SAWAAA!!!! KAIDI UONE

  2. abdulaziz says:

    HONGERA SANA DC ULEGA Ila jukumu kubwa ni kuhakikisha Bwege anarudisha Ubunge kwa CCM na Idadi ya madiwani,Mitaa,Vijiji vingi virudi..SAWAAA!!!! KAIDI UONE

Leave a Reply