Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA KYAKA-BUGENE, APONGEZA WANAHABARI WA KAGERA KWA KAZI NZURI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali wa mkoa wa Kagera ambao waliongozana naye katika ziara yake ya siku sita mkoani humo. Rais Kikwete amewapongeza wanahabari hao na kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri ya kuufahamisha umma kila hatua ya ziara yake kwa ufasaha na weledi.
Wanahabari hao pia wamefurahi kuona kwamba Rais hakuja na jopo la wanahabari kutoka Dar es salaam kwa kuwaamini wao, hatua anbayo  wamesema imewapa faraja na furaha kubwa na  kujiamini zaidi.
PICHA NA IKULU

This entry was posted in

Leave a Reply