Google PlusRSS FeedEmail

JAPAN YATANGAZA SERA MPYA KWA TANZANIA

*Tanzania sasa kuwa nchi lengwa ya Japan
*Kuisaidia kuwa kitovu cha uwekezaji Afrika
*Japan kushiriki maboresho Reli ya Kati
*Kupanua na kuboresha Bandari ya DSM
*Viwanda kikiwemo cha pikipiki za Honda kujengwa nchini
*Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan
DAR ES SALAAM, Tanzania
JAPAN imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambapo itaifanya kuwa nchi yake lengwa na kuiwezesha kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika.

Japan imedhamiria kuchukua hatua hiyo  kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, na theNkoromo Blog kuipata, imesema, uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013.

Kwa mujibu wa taarufa hiyo, uamuzi na msimamo huo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo,Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Taariufa imesema, kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya uboreshaji wa Reli hiyo.

Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi na kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Waziri huyi pia amesema kuwa moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.

Kwa kuanzia amesema kuwa kampuni mbili za Honda na Panasonic zimekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.

“Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan  katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania,” Motegi amekaririwa katika taarifa hiyo akimwambia Rais Kikwete.

Waziri huyo pia amesema kuwa baadhi ya kampuni za Japan zina mipango ya kuwekeza katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa hapa nchini.

Taarifa ya Ikulu imesema, wakati wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.

"Uamuzi huo wa Japan na ziara ya Motegi inakuja wiki na miezi michache baada ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania zinavyokubalika duniani", imesema taarifa hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply