Google PlusRSS FeedEmail

RIDHIWANI AANZA KUSAIDIA WADAU, AKABIDHI VITANDA 167 KWA SHULE SABA JIMBONI MWAKE, AAHIDI KUMALIZIKA TATIZO LA UMEME CHALINZE

 Mbunge wa Chalinze, mkoa wa Pwani, Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, akijaribu kimoja kati ya vitanda 267, kabla ya kuvigawa kwa shule saba za jimboni Chalinze, katika hafla iliyofanyika jana, kwenye shule ya Sekondari Lugoba jimboni humo. Shule zilizopewa vitanda hivyo vikiwa na magodoro yake, idadi ya vitanda ilivyopata ikiwa kwenye mabano ni; Chalinze (50), Moreto (50), Mandera (25), Talawanda (24), Kiwangawa (50), Lugoba (38) na Kikaro (30). Kwa mujibu wa Ridhiwani mgawo huo ni wa awamu ya kwanza.
 Ridhiwani akimkabidhi vitanda  50 Mwalimu Emmanuel Kahabi kwa ajili ya shule ya Chalinze. Kushono ni Abubakari Mlawa wa Kampuni ya MM Steel iliyotoa vitanda hivyo
 Abdalla Sakasa wa Lugoba- akikabidhiwa vitanda vitanda 38
 Charles Mussa wa Talawanda- vitanda  24
 Justin Nguma wa Moreto  vitanda 50
 Omari Msami wa Kikaro-vitanda 30
 Rose Umila wa  Mandera Girls vitanda 25
 Saidi Ally wa Kiwangwa akipongezwa na wadau baada ya kupata vitanda 50.
 Ridhiwani akifurahi na wanafunzi wa shule ya Talawanda baada ya kukabidhi vitanda kwa mwalimu wa shyle hiyo (kulia)
 Mgawo awamu ya kwanza
 Ridhiwani akizungumza na wadau kueleza mikakati mbalimbali ya kukwamua maendeleo ya jimbo la Chalinze, ambapo alieleza kuwa miongoni mwa vipaumbele ni huduma za umeme ambapo italetwa Transfoma itakayowezesha jimbo hilo kupata umeme wa uhakika, afya na elimu
Wadau wakimsikiliza Ridhiwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply