Google PlusRSS FeedEmail

WAZIRI WA ARDHI PROFESA ANNA TIBAIJUKA ASIFU KAZI INAYOFANYWA NA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akipokewa na Felic Maagi Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakati alipowasili kwenye Banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam leo. 2 
Mmoja wa watu waliotembelea banda la NHC akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo kutoka kulia ni Nalindwa Norbert, Rhobi Wambura na Wilson Sanane. 5 
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akzungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda hilo kushoto ni Bw. Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha NHC.
.......................................................................................
1.Nalipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwapatia wananchi makazi bora. Sisi upande wa Serikali tutaendelea kuwasaidia kisera ili waweze kutimiza wajibu wao vizuri zaidi. 2. Pamoja na ujenzi wa nyumba wanaoufanya katika maeneo mbalimbali nchini na kwa watu wa vipato vya chini na watu wa vipato vya kati na juu, Serikali inaupongeza mpango wa Shirika waliouanza kwa kasi wa kujenga nyumba za gharama nafuu nchini, mpango unaoendeshwa kwa kaulimbiu ya “nyumba yangu, maisha yangu” 3. Nyumba hizo sasa zimekamilika katika maeneo 14 ya Halmashauri za miji ikiwemo Mkinga(Tanga), Mvomero(Morogoro), Mnyakongo-Kongwa(Dodoma), Mkuzo (Songea), Mtanda(Lindi), Mrara(Babati), Unyankumi(Singida), Kibada na Mwongozo (Kigamboni), Bombambili(Geita), Ilembo na Inyonga(Katavi), Uyui(Tabora), Longido na Monduli(Arusha) na Mlole(Kigoma). Miradi mingine ya aina hii imeanza kutekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za Miji na Wilaya hapa nchini, lengo likiwa ni kufikia Mikoa yote na ikibidi kila Halmashauri nchini. 4. Ili kuufanya mpango huu mzuri wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kuwa endelevu, mambo kadhaa ni lazima yafanyike:- Kwanza ni kwa Halmashauri kote nchini kuunga mkono kwa kulipatia Shirika maeneo ya kujenga nyumba hizo yasiyokuwa na masharti magumu. Ardhi isifanywe kitegauchumi na Halmashauri kwa kuiuza kwa gharama kubwa kwani kufanya hivyo kutafanya nyumba zinazojengwa kuwa aghali. Pili, Halmashauri na wananchi kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kununua nyumba zinazojengwa na NHC ili mapato yatakayopatikana yawezeshe kujenga nyumba zingine kwa ajili ya wananchi. 5 Zipo pia nyumba zinazojengwa katika miji mikubwa “satellite cities” zenye lengo la kuwapatia wananchi makazi na kuondoa msongamano wa magari mijini. Miji hiyo ni pamoja na Burka, Usar River na Mateves Arusha, Luguruni, Kunduchi Rifle Range, Uvumba na Kawe - Dar es salaam. Aidha, katika mikoa kadhaa hivi sasa majengo makubwa ya biashara yanajengwa ili kuipa sura mpya miji yetu na kukuza shughuli za kibiashara. 6. Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, nalihimiza Shirika hili liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. 7. Nawasihi watanzania watembelee banda hili la NHC ili wapate taarifa za kina za namna ya kununua nyumba na mahali nyumba hizo zilipo.

This entry was posted in

Leave a Reply