Google PlusRSS FeedEmail

KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM YAKUTANA KUHOJI WAGOMBEA WA JUMUIYA HIYO NGAZI YA TAIFA.

Daud Msungu (kushoto)-Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara), Matulanga (wapili kushoto)-mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa Dar, Lihami na Mgombea mwingine kutoka Dar es salaam, wakiwa wanajadili jambo nje ya ukumbi wa white house uliopo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jijini Dodoma, leo tarehe 08 sept 2012.

Wagombea mbalimbali wa Jumuiya ya Umoja wa vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakiwa nje ya ukumbi white house, tayari kwenda kwenye mahojiano na Kamati ya Utekelezaji ya Taifa ya Umoja huo iliyokutana leo tarehe 08 sept 2012.

wagombea wakibadilishana mawazo kabla ya kukutana na kamati ya utekelezaji ya Taifa ya Umoja wa Vijana CCM, ambapo watahojiwa juu ya Nafasi mbalimbali za ngazi ya Taifa walizogombea katika Umoja huo.

Wagombea mbalimbali wa Uongozi wa Jumuiya Ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakiwa katika picha ya Pamoja Nje ya Ukumbi wa whitehouse uliopo katika Ofisi za MakaoMakuu ya Chama hicho, Jijini Dar es salaam,leo tarehe 08 Oct 2012. Wagombea hao wapo Dodoma kukutana na Kamati ya utekelezaji ya Taifa ya Umoja Huo kwa ajili ya mahojiano juu ya Nafasi hizo walizogombea ambazo ni nafasi ya M/kiti, Mkamu M/kiti, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Vijana Taifa pamoja na Wajumbe wa Baraza kuu la Vijana Taifa.

This entry was posted in

Leave a Reply