Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI BORA KATIKA SERA ZA KILIMO NA CHAKULA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa  Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za  kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.  Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora  za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na  Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.

This entry was posted in

Leave a Reply