Google PlusRSS FeedEmail

Serikali ya Japani yatia sahihi mikataba ya kusaidia Ujenzi wa Mabweni 4 wilayani Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi Msaada Unaogharimu USD 243.6

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Nachingwea,Arbogast Kiwale akiwa pamoja na Balozi wa Japan
Nchini Tanzania ,Masaki Okada wakitia saini mkataba wa kusaidia Ujenzi
wa Mabweni mawili ya shule ya  sekondari ya kutwa ya wasichana
Nachingwea wenye thamani ya dola za marekani 243,698. Mkataba huo
umesainiwa leo mbele ya Wabunge wa mkoa wa Lindi,Wakuu wa
wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri huku Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Katibu
Tawala mkoa akishuhudia.

Wabunge wa Mkoa wa Lindi nao wakishuhudia kuwekwa
kwa saini mikataba ya Kusaidia ujenzi wa Mabweni 2 ya shule ya
sekondari ya Nkowe wilayani Ruangwa Pamoja na Mabweni mawili ya Shule
ya kutwa ya wasichana Nachingwea.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkowe wilayani Ruangwa Mwl
Shannel Nchimbi akikabidhi  hati ya makubaliano ya msaada wa mabweni 2
kwa shule hiyo kwa Balozi wa Japan,Masaki Okada hii leo katika ukumbi
wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Serikali ya Japan imetoa Jumla ya dola za kimarekani 243,698 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni 4  kwa shule za sekondari za Nkowe wilayani Ruangwa Na Shule ya kutwa ya Wasichana wilayani Nachingwea Hatua hiyo imekuja katika jitihada za Nchi ya Japan kukuza Ushirikiano na Tanzania Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada leo amelala wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo kesho atatembelea shule ya sekondari NKOWE na Baadae kuelekea Wilayani Nachingwea

Picha na Habari toka kwa Mdau Abdulaziz video rec.

This entry was posted in

Leave a Reply