Google PlusRSS FeedEmail

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein aendelea na Ziara yake ya Kichama katika Mikoa ya Zanzibar

Na Mwinyui Sadallah Zanzibar


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Sheina amesema baadhi ya watu wakwermo wanasiasa wanaojaribu kubeza na kukejeli harakati za chama cha Afro Shriaz Party (ASP ) kilicholeta ukombozi visiwani Zanzibar historia itawahukumu.

Kauli hiyo aliitoa leo mara baada ya kufungua Tawi la CCM lililofanyiwa ukarabati ambalo lilijengwa mwaka 1963 huko Mzurikaja Makunduchi Mkoa wa Ksini Unguja .

Dk Shein alisema Zanzibar ilitawaliwa na utawala wa kisultan uliolindwa na Waingereza kwa karne nyingi hadi yalipofanyika Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Akisifu juhudi za wanasiasa toka Makunduchi ambao waliojitolea kwa nguvu na maarifa yao kukijenga chama cha ASP aliwataja ni pamoja na Hayati Idrisa Abdul Wakili na Hasnu Makame ambao walijitolesa maisha yao kupinga ukolini.

“Wazee wetu hao pamoja na wenzao walifanya kazi kubwa ya kukijenga chama cha ASP walipinga umwinyi, ubwenyenywe na usultani hadi ukombozi kamili ulipopatikana Zanzibar”Alisema Dk Shein.

Aidha aliwataka wananchama na viongozi wa Tawi hilo kukusanya kumbukumbu ya picha,kuchora na kuweka kumbukumbu ya historia ya chama cha ASP kwa faida ya kizazi kijacho.

“Kusanyeni na kuhifadhini kumbukumbu za ASP , wekeni na choreni picha kwa ustadi ili kuweka na kuonyesha ukweli ulivyo na ulivyukuwa kuhusu harakati za chama chetu,mkiacha kufanya kazi hiyo wanasiasa uchawara watapotosha ukweli”Alisema Dk Shein.

Dk Shein amabaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alisema sababu ya kufanya hivyo ni kulinda histria ya harakati zetu kwa kuwa kwa kuwatahadhari wanasiasa wazushi na na matapeli.

“Kuna wanasiasa ambao kazi yao si kunadi sera zaa vyama vyao ,ni wachekeshaji, hodari wa kuzua na kupotosha mambo, hupenda uzushi,ghiliba na ulaghai wanapokuwa kwenye majukwa ya kisiasa”Alisema Dk Shein huku akishangiliwa na wananchi.

Akizungumzia changamoto ya ajira na maji alisema hakuna mwanasiasa yeyote mwenye jibu la mkato katika tatizo la ajaira na kusema ukosefu wa ajira unazikali nchi nyingi duniani kwa wakati huu.

Alisema kati ya watu 100 kati yao 14 hawana ajira na hivyo kuwataka vijana kutoghilibiwa na soga za wanasiasa wanaojifanya wana uwezo wa kuleta ajira.

“Vijana msigombanishwe na chama chenu kwa kelele za wanasiasa matapeli,Serikali yenu iko mbnioni kuwaunganisha katika vikundi vya wajasiria mali ,mashirika yasio ya kiserikali, saccoss na vyama vya ushirika ili kujikwamua na tatizo la ajira”Alisema Dk Shein.

Kuhusu maji alisema SMZ imekopa kiasi cha shilingi bilioni 64.4 katika Benki ya Maendeleo Afrika pamoja Benki ya Dunia kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji na kuahidi kuliondoa tatizo hilo.

Alieleza kuwa mkakati wa serikali yake ni kuzitumia sekta rasmi na zisizo rasmi ili kuongeza ajira kwa vijana chini ya program ya kazi nje nje na kusema tayari mtaalam toka nchini India atawasili Zanzibar akitokea Rwanda..

End.



Na Mwinyi Sadallah ,Zanzibar

Rais wa Zazibar amewaaasa baadhi ya watu na wanansiasa wenye tabia ya kupenda kuchanganya dini na siasa kwa lengo la kuleta vurugu na ghasia kwa ni ya kuvunja misingi ya utulivu na amani iliopo visiwani Zanzibar.

DK Shein alitoa matamshi hayo huko Bwejuuu Mkoa wa Kusini Unguja mara baada ya kufungua Tawi lililofanyiwa matengenezo na kuingiza wananchma wapya 86 wa Chama Chsa Mapinduzi na jumuiya zake.

Alisema nia na dhamira ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingin vya siasa nchini ulikusudia kutaka kustawisha misingi ya demokrasia na wala si kuleta hasama, vurugu na uvunjifu wa amani uliopo.

“Serikali za CCM ndizo zilizofungua milango ya demokrasia kwa nia njema,anaetaka kuchanganya dini na siasa ili avuruge amani atapambana na vyommbo vya sheria na wala hataaachiwa atambe”Alisema huku akishangiliwa na wananchi,

Dk Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alisema hakuna mtu atakaezuiwa asiamini na kufuate imani ya dini yake lakini akaasa kuwa hatalubali kuona vyama vya siasa vikifanya kazi ya dini na na nyumba za dini zikiwa wakala wa vyama vya siasa.

Aidha aliwael;eza wananchi kuwa haukuna mtu yeyote mwenye misuli ya kushindana na Serikali na kwamba serikali yake haigopi sharubu za mtu yeyote ikiwa mtu huyo ataamua kuvunja na kukiuka sheria zilizopo.

Alisema kutokana na ruhusa iliotolewa kwa muijibu wa sheria ysa kuwepo kwa vyama vingi vya siasa kusiwafanye wengine kujiopna ni wababe wakitisha wenzao na kwamba watakajaribu kufanya atakutana na mookono ya sheria na anae bisha afanya aone.

Alisema histria ya Zanzibar ni yenye fahari kubwa mbele ya macho ya dunia hivyo si vyema kwa watu kutaka kuivuruga kwa kisiangizi cha kuwepo kwa mfumo wa vyamam vingi kwa kufanya vitendo vya vurugu.

“Nchi yetu ina insaf na umaarufu mkubwa ulimwenguni,tumeanza kusifiwa tokea karne nyingi zilizopita,hata tulipounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa tumeendelea kupata sifa, hatutakubali kumuona mtu au kikundi chochote kikipoteza heshima hiyo kwa maslahi binafsi”Alisema Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

This entry was posted in

Leave a Reply