Google PlusRSS FeedEmail

TAMKO LA RAIS JUU YA TUKIO LA ARUSHA


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa
ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki
la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha,
limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.
Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu
katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na
tukio hilo la kigaidi.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka
mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria.
Kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia
Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote
Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma.
Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au
aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na
chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali
kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais
anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu
hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa
wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana
nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia
katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za
ujenzi wa taifa.
Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini
wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na
shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM

This entry was posted in

Leave a Reply