Google PlusRSS FeedEmail

MKURUGENZI WA FES NCHINI AIPONGEZA CCM KWA KUJENGA DEMOKRASIA NCHINI

Mkurugenzi Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch (Kulia)akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM -Bara Ndugu Philip Mangula,leo katika ofisi ndogo za CCM Lumumba.
SHIRIKA la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung (FES), limekipongeza na kukisifu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuendelea kujenga utawala bora na kujenga amani ya nchi.Akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula, Mkurugenzi Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch, alisema shirika lake linatambua juhudi na kazi inayofanywa na CCM katika ujenzi wa demokrasia na amani ya Tanzania.
Paasch alisema Tanzania ni nchi muhimu katika historia ya bara la Afrika hususan mchango wake katika ukombozi wa nchi zilizo kusini mwa Afrika, hivyo inapaswa kuwa mfano na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kihistoria kuhusu ukombozi. "Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania na nafurahi leo kukutana nawe kiongozi wa juu wa CCM, kwa niaba ya FES naahidi kuimarisha na kuedndeleza ushirikiano uliopo baina yetu na CCM na Tanzania kwa jumla," alisema. Kwa Upande wake Mangula, alisema katika kuhakikisha Tanzania inatunza kumbukumbu muhimu za kihistoria za bara la Afrika, kwa makubaliano na nchi zingine za bara hilo zimeamua kutenga eneo maalumu wilayani Bagamoyo kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha kumbukumbu hiyo.Mangula alimwambia mkurungenzi mkazi huyo kuwa tayari eneo hilo limeshapatikana na kwamba mchakato wa hatua zaidi katika kuelekea ujenzi wake kwa kushirikiana na nchi nyingine, unaendelea

This entry was posted in

Leave a Reply