Google PlusRSS FeedEmail

DIWANI WA CHADEMA ATOA TAARIFA ZA UONGO.

 

Na Samson Chacha,  Tarime.

Diwani wa Kata ya Turwa tarafa ya Inchage kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Charles Ndessi Mbusiro amelalamikiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akiwemo Mwenyekliti Amos Sagara , Mkurugenzi Mtendaji Fidelis Lumato,, Mhandisi wa Wilaya Kasim Shaban  na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gimunta Champion Traders bw, John Gimunta  kwa kutoa taarifa za Uongo za Kata Nyingine kwa Kudai kuwa Kampuni hiyo imelipwa zaidi ya  tsh Milioni 30 za Ujenzi wa Barabara mpya inayounganisha Vitongoji vya  Msati na Romori Km 1.5 kila Upande ambayo ipo Kata ya Sabasaba Wakati Kampuni hiyo haijalipwa Fedha hizo anazodai Diwani Ndessi ,

Wakitoa Ufafanuzi Ofisini kwake hapo Septemba 10 mwaka huu  Kuhusiana na Taarifa Walizodai za Uongo Zilizoandikwa na baadhi ya Vyombo vya habari  Jumatatu Wiki hii likiwemo  ( gazeti la Dira ) Viongozi hao wa Halmashauri Mwenyekiti Sagara na Mkurugenzi Mtendaji bw, Lumato na Mhandisi   Kasim  walisema kuwa " tumesikitishwa na taarifa zilizotolewa kwa Vyombo vya habari na Diwani wa Kata ya Turwa bw, Ndessi ya Kata nyingine ya Sabasaba, kuwa Halmashauri tumisha Mlipa Mkandarasai Gimunta Champion Traders  tsh Milioni kati ya 30,000,000/=  na Milini 50 ,000,000,/= za Ujenzi wa Barabara Mpya yenye Umbali wa KM 3 Kwa pande mbili zinazounganisha Vitongoji vya Msati na Romori na Kwamba Barabara  hiyo imejengwa Chini ya Kiwango huku akijua kuwa taarifa alizotoa ni za Uongo ",
 
Bofya hapa...!

This entry was posted in

Leave a Reply