Google PlusRSS FeedEmail

WAJUMBE WA BARAZA LA UWT TAIFA WAKUTANA DODOMA, KUPITISHA MAJINA YA WAGOMBEA.

baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini ajenda mbalimbali za kikao hicho.

Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mama Amina Nassor Makilagi(aliyesimama) akifafanua jambo katika Kikao cha Baraza hilo, wengine ni Viongozi wakuu wa Umoja huo Mwenyekiti, Makamu na Naibu katibu Mkuu.

wajumbe mbalimbali walioudhuria Kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Dodoma, Leo.Septemba 10,2012

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mama Sophia Simba akiwa anasisitiza jambo muhimu miongoni mwa ajenda za msingi kwenye kikao hicho, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa whitehouse, uliopo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma.

Wajumbe mbalimbali walioudhuria Kikao Cha Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

BARAZA Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT), limefanya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbali mbali za wanachama waliomba katika ngazi ya taifa na mikoa.
Aidha limepitisha mapendekezo ya wanachama walioomba nafasi mbali mbali ambazo zitafanyiwa uteuzi katika vikao vya Chama ngazi za mikoa na Taifa.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makillagi baraza hilo  lilifanya uteuzi katika kikao chake kinachoendelea katika ukumbi wa Sekretarieti wa makao makuu ya CCM , Mjini Dodoma.
Amina alisema nafasi ya Mwenyekiti wa UWT wamependekeza majina matatu kati ya tisa ambapo mapendekezo hayo yatapelekwa kwenye vikao vya Chama vitakavyofanyika hivi karibuni.
Alisema pia katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti yamependekezwa majina ya wanachama watatu na katika nafasi halmashauri kuu ya taifa ambayo ina nafasi 15 yamependekezwa majini 45.
Aidha alisema wamependekeza majina ya wanachama walioomba nafasi za mwenyekiti katika ngazi za mikoa, wajumbe wa baraza kuu na halmashauri ya CCM mkoa.
Kwa upande wa uteuzi, alisema Baraza Kuu limefanya uteuzi wa wagombea 30 wa nafasi ya ujumbe wa baraza kuu la UWT taifa ambapo nafasi zinazowaniwa ni 10.
Pia wamefanya uteuzi wa wagombea kwa nafasi za uwakilishi kutoka UWT kwenda Jumuia za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Wazazi kwenye mikoa yote ya Bara na Visiwani Zanzibar.
Kikao cha baraza kuu kinaendelea ambapo idara ya Uchumi na Fedha itawasilisha taarifa yake pamoja na mpango kazi wa jumuia hiyo kwa mwaka 2009/2012 hapo kesho tarehe 11 Sept 2012.

This entry was posted in

Leave a Reply