Google PlusRSS FeedEmail

DKT BILAL AZINDUA KAMPEZI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUBUBU.

Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakati alipokuwa akizindua Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji, mjini Unguja jana Sept 02, 2012. Picha na OMR

Mbunge wa Iramba Magharibi, ambae pia ni Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Uchumi na fedham Ndugu Mwigulu Nchemba akiongea na kutema cheche katika mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni ambapo pia alimvisha Mgombea wa CCM, ndugu BHAA skafu ambayo kwayo  ikiwa ni ishara ya heshima  na kuvua utambulisho wake na kumtunuku mgombea huyo.
Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa mjini Unguja-Zanzibar, wakati alipokuwa akizindua Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo
 Mashabiki na wanachama wa CCM, wakishangilia na kufurahia hotuba ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao kwenye sherehe za uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo.

This entry was posted in

Leave a Reply