Google PlusRSS FeedEmail

MAJARIBIO YA TOWN-TRAIN,MKAKATI WA KUPUNGUZA MSONGAMANO DAR.

 Treni ya Abiria ambayo ipo kwenye majaribio, ambapo itakuwa inafanya shughuli ya usafirishaji wa abiria kutoka katikati ya jiji mpaka eneo la Ubungo, hatua hii imekuja ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi katika kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la msongamano wa watu na magari katika maeneo ya katikati ya jiji ambapo husababisha foleni kubwa katika Jiji la Dar es salaam. Mradi huu unategemea kukamilika na kuanza kazi rasmi mwishoni mwa mwaka huu. Kulingana na Maagizo ya Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi, Mheshimiwa Dr. Harrison Mwakyembe, Treni hiyo inatakiwa kuwa kiunganishi na tegemezi kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la Usafiri kutokana na kuwepo kwa foleni na msongamano mkubwa wa watu na magari katikati ya Jiji. 

This entry was posted in

Leave a Reply