Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama
Katika Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akisoma utangulizi, mwanzoni wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa
Wajumbe wa Kamati Kuu, Maua Daftari na Simba wakijadili jambo taratibu, kabla ya Kikao cha kamati hiyo kuanza leo mjini Dodoma
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wa Kamati Kuu, Shamsi Vuai Nahodha na Spika Pandu Ameir Kificho wakiwa kwenye kikao hicho na kulia ni Dk. Abdallah Kigoda.Baadhi ya viongozi wa CCM wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi kwa awamu nyingine katika uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika Novemba mwaka huu, wakiwa nje ya ukumbi wakati kikao cha Kamati Kuu kikiendelea mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Azim Premji, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus-Rukwa, Wajumbe wa NEC Asha Baraka na Hkadija Kopa
Anthony Dialo (kulia) akijadili jambo na wenzake nje ya ukumbiKina William Lukuvi, Tyson (siyo wa ngumi) na Nchemba wakibadiloishana mawazo nje ya ukumbi kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO