Google PlusRSS FeedEmail
 Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata ya Lupa, wilayani humo.
 Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 "Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
 "Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson wakati akilivua  gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto).
 Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
 Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa.  Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha

KABLA YA HAPO KINANA ALIKAGUA UJENZI BARABARA YA MBEYA-CHUNYA HADI TABORA INAYOJENGWA NA KAMPUNI YA CCCC YA CHINA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikagua sehemu ya ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya inayoenda hadi Tabora, unaofanywa na Kampuni ya Kichina ya CCCC, wakati Kinana na msafara wake walipokuwa wakipita katika eneo hilo, akiwa njiani kwenda wilayani Chunya, leo
 Baadhi ya maeneo yanajengwa kwa uhodari mkubwa kiasi kwamba kupita ni lazima kuruka, Hapa Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi akiruka kutoka upande mmoja kwenda mwingine wa eneo hilo linalojengwa.Nyuma yake ni Kinana ambaye naye alimfuata Nape pia kwa kuruka eneo hilo
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiruka eneo hilo
Kazi ya kuopasuka milima na kuweka sawa inapopita barabara hiyo, ikiendelea

MIKUTANO NA SHUGHULI NYINGINE ZA KINANA WILAYANI CHUNYA
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaslimia wananchi, baada ya msafara wa Kinana kuwasili wilayani Chunya
 Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kusimamia msafara wake akiwa njiani kwenda Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM katika kituo cha mabasi mjini Chunya.
 Kisha akakabidhi kazi za CCM kwa wanachama wapya 100 kwenye shina hilo
 Kinana akihutubia baada ya kizindua shina hilo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia) akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya
 Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lupa,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi mashine isiyotumia umeme, ya kufyatulia matofali, kwa kikundi cha wajasiamali, wakati wa mkutano wa hadhara aliofanya Nov 30, 2013, katika Kata ya Lupa, wilayani Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013. Wengine ni Mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Imatayarishwa na theNkoromo Blog

ZIARA YA KINANA WILAYANI CHUNYA MOTO, AMZOA KATIBU WA CHADEMA WA WILAYA HIYO, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, WANANCHI WAFURIKA KWENYE MIKUTANO YAKE

 Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi Kat... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
 Wananchi wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akihutoa dozi' alipohutubia katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa 'dozi' katika mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika  Uanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma,leo
Baadhi ya vijana wakiwa juu ya miti kuhakikisha wanaowaona viongozi wakati wa mkutano huo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati mwenye  miwani) akiselebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma leo
Kinana akizungumza na Kijana Martin Thomas (38) mjini Tunduru, aliyezaliwa bila mikono,mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa Mbozi Ndugu Zambi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiondoka Uwanjani baada ya mkutano huo kumalizika akiwa ametawazwa kuwa chifu wa moja ya makabila  maarufu ya Mbeya

MKUTANO WA KINANA TUNDUMA WAFUNIKA, MAELFU WAJITOKEZA, NAPE ABEBWA

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momb... [Read More]


 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na viongozi wa wilaya ya Momba mkoani Mbeya, katika mpaka wa wilaya hiyo na Ileje leo saa 5 asubuhi.
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Momba mkoani Mbeya, katika mpaka wa wilaya hiyo na Ileje leo saa 5 asubuhi.
Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Momba, wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, alipokutana nao katika kikao cha ndani kwenye ukumbi wa Uwanji, wilayani humo, leo. Imetayarishwa na CCM BLOG

KINANA NA MSAFARA WAKE WATINGA WILAYANI MOMBA LEO ASUBUHI

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na viongozi wa wilaya ya Momba mkoani M... [Read More]

DUNIA MZOBORA
DAR ES SALAAM, Tanzania
MHARIRI Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

Habari zimesema Mzobora (49), ambaye alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi, akitokea Hospitali ya Aga Khan pia ya Dar es Salaam, anazikwa leo saa 7 mchana katika makaburi hayo

Mussa, mdogo wa marehemu, alisema jana kuwa Mzobora alianza kujisikia vibaya juzi usiku  nyumbani kwake,Tabata Mawenzi na kupelekwa Aga Khan, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na ndipo alipopelekwa Muhimbili. Alifariki muda mfupi baadaye wakati madaktari wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yake.

Mzobora, ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Naibu Msanifu Mkuu wa Uhuru, alifanya kazi hadi kumalizika kwa gazeti la Uhuru toleo la jana, akikaimu nafasi ya msanifu mkuu, akiwa buheri wa afya.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka kwa ndugu wa familia, zilisema maziko ya marehemu yatafanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mzobora, ambaye alizaliwa Aprili 6, 1964 Mwandiga mkoani Kigoma, alijiunga na Uhuru Publications Limited mwaka 1989, akiwa mwandishi wa habari mwanafunzi, baada ya kumaliza masomo ya ualimu ngazi ya cheti kutoka chuo cha Kasulu, mkoani Kigoma.
Kutokana na uwezo wake na kujituma kazini, mwaka uliofuata alithibitishwa kazini na kupandishwa cheo kuwa mwandishi kamili wa habari.

Mwaka 1992, alipandishwa cheo na kuwa msanifu kurasa wa Mzalendo na Burudani chini ya Msanifu Mkuu wa magazeti hayo kwa wakati huo, Hamisi Mkwinda, kabla ya kupandishwa na kuwa mwandishi wa habari daraja la pili mwaka 1994.

Mwaka 1995, alijiunga na kilichokuwa Chuo cha Uandishi wa habari cha Nyegezi (sasa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine), Mwanza na kuhitimu stashahada ya juu ya uandishi wa habari mwaka 1998.

Baada ya kurejea kazini, alipandishwa vyeo ngazi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi daraja la pili na hadi kufariki dunia kwake, alikuwa Mhariri Daraja la Pili.

Miongoni mwa nyadhifa alizoshika ni pamoja na Kaimu Msanifu Mkuu wa Uhuru, Kaimu Mhariri wa Mzalendo na Kaimu Mhariri wa Makala.

Kutokana na kiu yake ya kupenda elimu, mwaka 2006, Mzobora alijiunga tena na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Mwanza kwa masomo ya shahada ya uzamili katika mawasiliano ya umma na uandishi wa habari. Marehemu ameacha mke na watoto.

Wakati huo huo; Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za pole Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, kufuatia kifo hicho.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha mmoja wa Waandishi wa habari shupavu na mchapakazi, Dunia Mzobora aliyekuwa akilitumikia Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la UHURU,” alisema Rais Kikwete.

Alisema alimfahamu Mzobora, enzi za uhai wake, kama Mwandishi wa Habari aliyejituma katika kazi zake za kuuhabarisha, kuuelimisha na kuuburudisha Umma kwa kutumia vyema kalamu yake.

Katika salam hizo, Rais Kikwete ametoa pole pia kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru na Waandishi wote wa habari nchini, kwa kumpoteza mwenzao waliyekuwa wakifanya naye kazi kila siku.

“Aidha, kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu Dunia Mzobora kwa kumpoteza baba, kiongozi na mhimili wa familia,” alisema Rais Kikwete.

Amewahakikishia wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao, na anamuomba  Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu, Amina.

Amewataka wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia baada ya kumpoteza mtu muhimu aliyekuwa kiungo cha familia yao, kwani yote ni mapenzi yake Mola.

DUNIA MZOBORA KUZIKWA MCHANA HUU MAKABURI YA KISUTU, DAR ES SALAAM

DUNIA MZOBORA DAR ES SALAAM, Tanzania MHARIRI Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anazi... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi ya wodi y a wazazi ya kituo cha afya kata ya Lubanda wilayani Ileje.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishirikiana na wananchi wa kata ya Lubanda kujenga msingi wa wodi ya akina mama katika kituo cha afya cha kata hiyo wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwa nyumbani kwa Balozi wa Shina namba 1 Balozi Nosadi Edward (mwenye fulana kulia),Katibu Mkuu amekuwa na utamaduni wa kutembelea mabalozi katika ziara zake .
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na wakazi wa shina namba 1 kata ya Sange ,wilaya ya Ileje mkoan Mbeya.

Wasanii wa ngoma wakicheza ngoma ya Ibandi ngoma maarufu ya kabila la Wandari wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Ujumbe wake ambao walitembelea kata ya Kalembo ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
 Diwani wa Kata ya Isongole Ndugu Gwalusako Kapesa akielezea namna gani wananchi wa ilaya ya Ileje wamechoshwa na taratibu za serikali za kuwalazimisha kununua mbolea za ruzuku za Minjingu kwani zimekuwa hazina faida kwao kama wakulima na zimewaletea hasara kubwa sana, wananchi hao wameiomba serikali na viongozi wake kuwasikiliza zaidi wao katika kutatua kero zao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kalembo na kuwaambia kilio cha wakulima kinafanana karibia nchi nzima hasa kuhusu matatizo ya mbolea na kusema CCM itachukua hatua kwa kukutana na waziri husika kwenye kamati kuu itakayofanyika mapema mwezi ujao.
 Wananchi wa Kata ya Kalembo wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga na mvua wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ambao upo ziarani mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za kumbukumbu za kifo cha marehemu Steven Kibona kwa wananchi wa kata ya Kalembo, kushoto ni mjane wa marehemu Mama Kibona.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Rosemary Sinyamule kwenye daraja la mto Songwe mpakani mwa Tanzania na Malawi,Mkuu wa Wilaya alimueleza Katibu Mkuu kuwa kuna eneo hilo lina fursa nyingi kibiashara na kiuchumi kama barabara ya lami  itajengwa na ikiwa pamoja na ofisi za kudumu za uhamiaji zitajengwa katika kata ya Isongole.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakizungumza na wananchi wa kata ya Isongole wilaya ya Ileje mpakani mwa Tanzania na Malawi.
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa nje ya ofisi ya uhamiaji ya kata ya Isongile wilaya ya Ileje mkoani Mbeya,kushoto ni mkuu wa kituo hicho cha uhamiaji Ndugu  Fredrick Luhanga.

WAKULIMA WA ILEJE WAIKATAA MBOLEA YA MINJINGU

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi ya wodi y a wazazi ya kituo cha afya kata ya Lubanda wilayani Ileje... [Read More]


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake (katikati) wakiwa wamezungukwa na umati wa wananchi, Kinana alipokuwa akizindua Shina la Wakereketwa Wajasirimali wa Kikundi cha Amani na Maendeleo cha waendesha bodaboda, Katika Kata ya Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi  nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari Kaya ya Ikuti, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Wananchi katika Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Hayupo Pichani) huku wengine wakiwa juu ya miti ili kumuona kiongozi huyo wa CCM, katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Nov 27, 2013, katika kata hiyo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi wa Kata ya Masoko, Rungwe, mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akifurahia jambo na Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano uliofanyika katika jimbo hilo, Kata ya Masoko, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akimkumbatia kwa furaha Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano uliofanyika katika jimbo hilo, Kata ya Masoko,wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013
Wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika soko la Kata ya Ikuti, katika kijiji cha Butonga, wilayani, Rungwe, wakiwa wameacha biashara zao na kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana ili kumweleza kero zao, alipokuwa akipita eneo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua utelezaji ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujaliana nao njia bora ya kuzitatua, Nov 27, 2013.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipewa zawadi na Jane James, Mke wa Mjumbe wa Shina namba 2, Butonga, Kata ya Ikuti, Rungwe, James Mbasi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa mjumbe huyo, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza kijana  Asimwise mwantebele baada ya kijana huyo kutangaza kuhamia CCM akitokea Chadema, wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizindua shina la wakereketwa wa CCM la Kiwira, wilayani Rungwe, Nov 27, 2013.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akikabidhi mchango wake wa sh. laki moja (100,000) kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbozo Godfrey Zambi, kwa ajili ya kusaidia harakati za maendeleo ya kiuchumi kwa shina la wakereketwa wajasirimali waendesha bodaboda, wa CCM, katika Kata ya Kiwira, wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimhoji jukwaani, Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Crispian Meela (kushoto) ni kwa kiwango gani amesimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, wilayani kwake, wakati wa mkutano wa hadhara kata ya Ikuti, wilayani humo, mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na kinamama wauza ndizi wa  Iponjola, wilayani Rungwe mkoaoni Mbeya, Nov 27, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtambulisha Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, kwa kinamama hao wa  Iponjola, 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtambulisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa kinamama hao wauza ndizi wa  Iponjola, wilayani Rungwe mkoaoni Mbeya, Nov 27, 2013.

KINANA AWEKA HISTORIA YA KIPEKEE KATIKA ZIARA YAKE WILAYNI RUNGWE

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake (katikati) wakiwa wamezungukwa na umati wa wananchi, Kinana alipokuwa akizindua Shina ... [Read More]