Google PlusRSS FeedEmail

Na Mwandishi Maalum
Tanzania,  imeungana na mataifa mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa Mageuz iya Sekta za Usalama ( Security Sector Reform).

Akichangia majadiliano ya Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutana kwa siku nzima ya Jumatatu  wiki hii, kujadili taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu SSR,  Naibu Mwakilishiwa Kudumu wa Tanzania katika  UN, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi inapenda kuona kwamba mageuzi ya sekta za usalama yanamilikiwa na nchi zenyewe zikiwamo nchi zinazotoka katika machafuko.

Katika Mkutano huo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja na kwa mara ya kwanza Azimio linalojitegemea kuhusu mchakato wa Mageuzi ya Sektaza Usalama,kupitia azimio hilo namba 2151 (2014)  pamoja na kusisitiza umuhimu wa dha nazima ya mageuzi ya sekta za usalama na umuhimu wake kwa usalama, amani na ustawi wa mwanadamu.
 Azimio linasisitiza kwamba umiliki wa nchi katika mageuzi hayo ni jambo la muhimu.

Akaongeza kuwa makundi ya wapiganaji na ambao wameka silaha zao chini na kuingia katika mchakato wa majadiliano wanapaswa pia kuwa sehemu ya mageuzi ya sekta za usalama.

Akasema kwa kuyashirikisha makundi hayo ya wapiganaji na mengine kutasaidia ujenzi wa Amani na usalama na pia kuepusha kujirudia kwa mapigano.

Aidha Balozi Mwinyi, ameleza kwamba, nchi zinazopakana na nchi zinazotoka kwenye machafuko pia zinayo nafasi na wajibu wa kutoa ushirikiano na uzoefu wao katika ujenzi wa sekta za usalama.

Vile vile Balozi amebainisha kwamba katika miongo ya miaka mitano iliyopita imedhihirisha wazi umuhimu wa jumuia za kikanda katika uzuiaji wa mapigano, ulinziwa Amani naujenziwa Amani.

Majadiliano hayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na yaliitishwana Nigeria ambayo ni Rais wa Baraza hilo kwa Mwezi huu wa April. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria  Bw. Aminu Wali aliongoza majadiliano.

Wawakilishi kutoka nchi 42 wanachama waUmojawa Mataifa, zilizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhana hiyo ya mageuzi ya sektaza usalama, na bila ya kujali tofauti zao,  kila moja ilisisitiza hoja ya nchi kumiliki mchakato huo hata kwa zile ambazo zimetoka katika machafuko au mapigano.

Aidha pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa nchi kumiliki mchakatohuo, zimeongeza kuwa bado kuna haja ya Jumuiya ya Kimataifa,  kuziwezesha nchi hasa zile zinazotoka katika machafuko kuweza si kujenga upya sekta hizo za usalama bali pia kuzifanyia mageuzi.

Vile vile ilisisitizwa pia kuwa mageuzi hayo ya sekta za usalama ni muhimu katika kuziimarisha nchi ambazo ndiyo kwanza zimetoka kwenye machafuko. Na kwamba mageuzi hayo yatapewa kipaumbele katika utekelezaji mamlaka za ulinzi wa Amani  na misheni maalum za Kisiasa.

Wajumbe wengine walikwenda mbalizaidi, kwa kueleza kwamba mageuzi hayo ya sektza za usalama yanapashwa kuwajumuishi kwa maana ya kushirikisha makundi mengine ya kijamii. Lakini kwa msisitizo kwamba serikali ndiyo iwe na mamlaka ya kuamua mfumo wa sekta zake za usalama.

Katika salamu zake za ufunguzi Ban ki Moon,  alisema,  lengo la kutekeleza mageuzi ya sekta za usalama ambazo ni pamoja na jeshi, polisi na vyombo vya usalama ni kuwawezesha wananchi ambao ndiyo walengwa kuishi maisha yenye usalama.

“Sektaza Usalama ndiyo muhimili mkuu wa makubaliano kati ya serikali na wananchi wake. Mamlaka ya kutumia nguvu nilazima yaendane na wajibu wa kulinda raia na kuheshimu haki za binadamu” akasemaKatibuMkuu.

Kwa mujibu wa Ban Ki Moon,  sekta za usalama zinazotekeleza majukumu yake chini ya misigi ya utawala wa sheria zina uwezo wa kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao na hivyo kuchangia katika uimara wa ujenzi wa Amani namaendeleo.

NCHI ZIMILIKI MAGEUZI YA SEKTA ZA USALAMA: TANZANIA

Na Mwandishi Maalum Tanzania,   imeungana na mataifa mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa Mageuz iya Sekta za Usa... [Read More]

SURA YA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO APRILI 30, 2014

[Read More]

BODI ya Wakurugenzi  ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini. 
Uamzi huo umefanywa leo  (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw. Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Bw. Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na EWURA.

Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeundwa chini ya sheria ya EWURA, sura namba 414 ya Sheria za Tanzania. EWURA ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi  katika  sekta Nne (4)  za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

IMETOLEWA NA
BW. FELIX NGAMLAGOSI
MKURUGENZI MKUU
EWURA

EWURA YAFURA LESENI ZA KAMPUNI KUBWA TISA ZA KUUZA MAFUTA

BODI ya Wakurugenzi  ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Wh... [Read More]

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika kuwasilisha ujumbe wa Rais huyo kwa Rais Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaa leo April 29, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Sheikh Mohamed Rukara, ujumbe  maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza,
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya kalenda kutoka kwa Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Mama Lena Mfalila wakati alipokutana na uongozi wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo April 29, 2014. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif S. Rashid.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  na Viongozi wa  Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania
  Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati akizindua rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014
  Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati akizindua rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014
 Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati akizindua rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014
 Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama alama ya kuzindua  rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014
Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama alama ya kuzindua  rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014 
Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama alama ya kuzindua  rasmi  rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014. PICHA ZOTE NA IKULU

KIKWETE ACHAPA KAZI TATU KWA MPIGO LEO, AKUTANA NA MJUMBE WA RAIS WA BURUDI, VIONGOZI WA BARAZA LA UUGUZI NA KUZINDUA MKOBA PRIVATE EQUITY FUND

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika kuw... [Read More]

Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam
 Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam
 Mshana akipewa zawadi
 Wadaiu waliohudhuria
 Wadau waliohudhuria


Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua r... [Read More]