Google PlusRSS FeedEmail

KINANA KUFUNGA KAZI MKUTANO WA MWISHO SUMBAWANGA LEO

Sumbawanga, Tanzania
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, leo anahitimisha ziara yake katika mkoa wa Rukwa kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini hapa.

Mkutano huo utakaofanyika kuanzia mida ya tisa alasiri, unatarajiwa kuhudhuriwa na waelfu ya watu, kutokana na wananchi wengi kuonekana kupania kuhudhuria lengo kubwa likiwa ni shauku yao ya kutaka kumuona na kumsikiliza Katibu Mkuu huyo wa CCM.

"Lazima nihakikishe nafika kwenye kumsikiliza Kinana kwenye mkutano huo, maana nasikia huwa hamung'unyi maneno anapozungumzia kero za wananchi kwenye mikutano ya hadhara", alisema Protas Kaimbe, mkazi wa mtaa wa Majengo mjini Sumbawanga.

Kauli kama hizo za kupania kumuona na kumsikia Kinana zimekuwa zikitamkwa mjini hapa na watu kwenye migahawa na vijiwe mbalimbali hasa vya vijana, tangu jana na leo.

Akiwa mkoani Rukwa ambako aliwasili Machi 30, 2014, Kinana ametembea katika wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga Vijijini ambako alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara na kukagua shughuli za ujasiriamali katika nyanja kadhaa na utekelezaji wa ilani ya CCM.

Baada ya kumaliza ziara yake mkoani Rukwa, Jumanne hii ataanza ziara nyingine katika mkoa wa Kigoma na baadaye kwenda mkoa mpya wa Katavi.

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Ushauri tunaomba mkjutano huo urushwe kwenye TV

Leave a Reply