Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jana, aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Rukwa, kwa kutembelea wananchiwalioko pembezoni mwa mkoa huo, ambapo alifika hadi katika Kata ya Wampembe iliyopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilaya ya Nkasi ilimo kata hiyo.
Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara kwenye tope na makorogoro kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.
Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na hivyo kuwa vigumu kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo. Pichani Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko kwenye ziara hiyo.

Wananchi wa Kijiji cha Wampembe wakijimwayamwaya kwenye mkutano wao na Kinana

Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Nyuma yake ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka

Kinana mama, baba na watoto wakimpokea kwa hamasa kubwa Kinana katika kijiji cha Wampembe

Wananchi katika kijiji cha Ntemba Kata ya Kate wilayani Nkasi wakimsikiliza Kinana, alipoamua kuzunguza nao baada ya kumzuia njiani akitoka Wapembe kwenda Sumbawanga
CHANGAMOTO ZA BARABARA

Kinana akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara wake kunasa kwenye pori la akiba la Nkasi, wakati akitoka Kata ya Wampembe



MTI WA NGUVU ZA KIME
Waandishi wa habari kwenye msafara wa Kinana akishangaa mti ambao unakarinia kuanguka kutokana na kumegwa vbanzi na watu wanaoamini kwa vibanzi kutoka mti huo ni dawa ya nguvu za kiume. mti huo upo pembeni mwa barabara ambako magari ya msafara wa Kinana yalinasa wakati wa kwenda na kutoka kijiji cha Wampembe.
Jamaa akigema kibanzi kwenye mti huo. Imetayarishwa na Bashir Nkoromo wa CCM Blog