Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA KINANA WILAYA YA MLELE


  • Atembelea kata ya Kibaoni, asalimiana na wananchi na kukagua mradi wa maji, akutana na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda .
  • Ajionea mradi wa ufugaji Nyuki katika shamba la Waziri Mkuu

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Wazee wa kijiji cha Majimoto kata ya Majimoto baada ya kupewa heshima ya kuwa Mzee wa Kijiji hicho kwenye viwanja vya michezo vya Majimoto sehemu ambayo mkutano wa hadhara ulifanyika na kuhudhuriwa na umati mkubwa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasomea wakazi wa kijiji cha Majimoto vijiji vitakavyopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Mlele .

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Majimoto ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa sera kabisa za kuzungumza na kuanza kuwatukana waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwataka wananchi kutowapa nafasi wanasiasa ambao hawana sera za maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mama wa Waziri Mkuu Pinda,Albertina Kasanga wengine waliongozana na Katibu Mkuu alipomtembelea Mama wa Waziri Mkuu ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Balozi Ali Abeid Karume, Katibu Mkuu alifika kumsabahi Mama wa Waziri Mkuu wakati wa ziara yake katika wilaya ya Mlele,aliyekaa kushoto kwa Mama ni mdogo wa Waziri Mkuu Ndugu Wofgaga Pinda.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


This entry was posted in

Leave a Reply