NA BASHIR NKOROMO, KIGOMA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kutua Kigoma kesho, kuanza ziara ya siku tano mkoani hapa.
Ratiba iliyotolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga, inaonyesha kuwa mapokezi ya Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma, uliopo eneo la Kipampa, Ujiji yatafanyika kuanzia saa 3.00 asubuhi na kumalizika saa 4.00 asubuhi.
Kulingana na ratiba hiyo, baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Kinana ataenda Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma, ambako atafanya shughuli kadhaa ikiwemo kusaini kitabu cha wageni na kupokea taarifa ya Chama, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya mkoa na baadaye kufungua mradi wa maduka.
Baada ya kupumzika kati ya saa 6. 00 hadi saa 7. 00 mchana, Kinana ataondoka na msafara wake kwa njia ya boti kupitia ziwa Tanganyika, kwenda Hifadhi ya Taifa ya Gombe ambako atatembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kufahamu changamoto na mafanikio zilizopo kwenye rasilimali hiyo ya nchi.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa, Aprili 9, 2014, Kinana atakwenda wilaya ya Kasulu ambako baada ya kusaini kitabu wilayani na kuzungumza na katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya hiyo, atafanya shughuli kadhaa katika Kata mbalimbali.
Kinana anaaza ziara hiyo, baada ya juzi kumaliza nyingine ya siku sita katika mkoa wa Rukwa, ambako katika ziara hiyo alikagua uhai wa chama, utekelezaji wa ilani na Chama na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia za kuzitatua pale zilizpojitokeza.
Wakati huohuo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pia anatarajiwa kutua mkoani Kigoma, kesho asubuhi, kuungana na Kinana kwenye ziara hiyo.
Nape anaungana na Kinana baada ya kumaliza shughuli pevu ya kuratibu kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze. Kampeni hizo zilimalizika juzi na uchaguzi wake kufanyika jana ambapo CCM imeibuka kidedea kwa kuzoa kura nyingi.
Kutokana na CCM Blog kupata fursa ya kuwepo Kigoma, itakuwa ikijitahidi kuwahabarisha hasa kwa picha matukio yatakayoambana na ziara hiyo ya Kinana.
©2014 CCM Blog
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2014
(556)
-
▼
April
(68)
- NCHI ZIMILIKI MAGEUZI YA SEKTA ZA USALAMA: TANZANIA
- SURA YA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO APRILI 30, 2014
- EWURA YAFURA LESENI ZA KAMPUNI KUBWA TISA ZA KUUZA...
- KIKWETE ACHAPA KAZI TATU KWA MPIGO LEO, AKUTANA NA...
- TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAF...
- MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI
- ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KATA YA KAWE Y...
- SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA M...
- MWEMBE ULIOPANDWA NA NYERERE NA KARUME KATIKA IKUL...
- HONGERA WATANZANIA KWA KUADHIMISHA KWA KISHINDO MI...
- VIJANA WAFANYA MATEMBEZI YA UZALENDO
- KINANA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA MSUMBIJI JIJINI D...
- CCM TAWI LA UINGEREZA WAUNGANA NA WATANZANIA KUADH...
- NAPE AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA KIMAREKANI
- MTUMISHI UHURU FM, CECY JEREMIAH APATA MSIMA MZITO
- MZEE CLEOPA MSUYA ANG'ATUKA RASMI KATIKA UONGOZI W...
- TANZANIA: TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA MAT...
- WAZIRI MKUU AREJEA DODOMA LEO KUENDELEA NA BUNGE M...
- MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA 28 N...
- CHADEMA: KIKWETE NI JEMBE KATIKA MAENDELEO
- KATIBU MWENEZI WA CHADEMA WILAYA YA MEATU AHAMIA R...
- TAMASHA LA PASAKA LATIKISA UWANJA WA TAIFA
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUFUNGUA KONGAMANO LA M...
- TANZANIA NI NCHI YA AMANI
- KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KATAVI
- KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA MLELE
- MVUA KUBWA KUENDELEA KUNYESHA WANANCHI WATAKIWA KU...
- KINANA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA 60 ZA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSI...
- ZIARA YA KINANA WILAYA YA MLELE
- CCM YAZIDI KUIMARIKA NA KUAMINIKA
- KINANA AANZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE MKOANI KATAVI
- TAARIFA MUHIMU KUTOKA TAWI LA CCM UINGEREZA
- KINANA AHUTUBIA BILA KUJALI MVUA KIGOMA MJINI
- WAVUVI KIBIRIZI WATOA YA MOYONI KWA KINANA
- TAHADHARI YA MVUA KUBWA
- KINANA, NAPE WAFANYA MAMBO MAZITO JIMBONI KWA ZITT...
- KINANA AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE WILAYANI BU...
- DHANA YA KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA
- KINANA ANA KWA ANA NA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA
- ZIARA YA WILAYA YA KASULU MKOANI KIGOMA YAFANA, MA...
- KINANA AKAGUA MRADI WA MAJI KASULU
- NYANGWINE KUWASHITAKI KWA KINANA MAKADA WANAOMHUJU...
- KINANA ATUA KIGOMA KUANZA ZIARA YA SIKU SITA MKAON...
- KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA KATIKA SHUGH...
- KINANA, NAPE KUTUA KIGOMA KESHO ASUBUHI
- RIDHIWANI KIKWETE KIDEDEA, CCM YAPATA USHINDI WA K...
- RAIS JAKAYA APIGA KURA MSOGA
- MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UBUNGE CCM JIMBO LA ...
- KINANA AMALIZA ZIARA MKOANI RUKWA KWA KUHUTUBIA MA...
- MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO WA CHALIZNE KAMILI KWA A...
- SHIVJI: SIFUATI MATAKWA YA WANASIASA
- KINANA KUFUNGA KAZI MKUTANO WA MWISHO SUMBAWANGA LEO
- RIDHIWANI AITEKA KATA YA PERA
- RIDHIWANI KUWA MBUNGE WA VITENDO JIMBO LA CHALINZE
- KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI LE...
- VYAMA VYASHAURIWA KUWATUMIWA MAWAKALA WA JIMBO HU...
- RIDHIWANI AHUTUBIA WAKAZI WA KATA YA BWILINGU CHAL...
- TAASISI YA BRIEN HOLDEN KUZINDUA HUDUMA YA UPIMAJI...
- ZIARA YA KINANA KATIKA WILAYA MPYA YA KALAMBO MKO...
- UONGOZI WA JUU CHADEMA WAMTELEKEZA MGOMBEA WA CHAM...
- ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE KUFIKIA UCHAGUZI WAPIN...
- NAPE:CCM INA UHAKIKA NA USHINDI CHALINZE
- TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
- KINANA AFIKA MAENEO YA PEMBEZONI NKASI, AKUMBANA N...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APANDA MTI KUADHIMISHA S...
- MWELEKEO WA KIMBUNGA "HELLEN" NA HALI YA MVUA
- RIDHIWANI KUANZA NA BARABARA KISHA ELIMU NA AFYA T...
-
▼
April
(68)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.