Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi (Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

Eneo la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.

Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania

Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo

'Obama' akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo Kata ya Buhigwe.
Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo

Nape akiwa amezungukwa na watoto wa Kijiji cha Kibande, wakati akifanya kazi zake kwenye kompyuta pambeni mwa mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kijiji hicho kata ya Buhigwe

Baadhi ya matangazo kwenye mpaka huo


Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Munanila wilayani Buhigwe.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana, Munanila, Buhigwe

