Google PlusRSS FeedEmail

TANZANIA: TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA MATAIFA KATIKA ULINZI WA AMANI

Balozi Mwinyi
Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kuhusu ujumuishwaji katika mchakato wa  uboreshaji wa  taasisi za usalama (SSR), iliyofanyika Jumanne wiki hii, katika  Uwakilishi wa Kudumu wa  Japan kwenye Umoja wa Mataifa kwa kuandaliwa kwa ubia kati ya Japan, Tanzania na Slovakia. Na Mpigapicha Maalum
-------------------------------------------------
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imeihakikishia  Jumuiya ya Kimataifa kwamba itaendelea kushirikiana na   Umoja wa Mataifa  na  Jumuiya   za Kikanda  katika  jitihada za  urejeshwaji na uimarishaji wa mazingira ya amani na usalama katika nchi zenye migogoro.

 Kauli  hiyo imetolewa na   Balozi Ramadhani Muombwa  Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa   Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa, wakati   wa  ufunguzi wa  semina ya   siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano  kati ya Balozi za Japan, Tanzania na Slovakia.

Mada kuu  ya semina  hiyo  iliyofanyika siku ya jumanne  katika  Ubalozi wa Japani hapa Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na  wawakilshi kutoka  Balozi mbalimbali, watendaji kutoka Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine , ilihusu Ujumuishwaji katika Ujenzi wa Nchi,  Inclusivity in  Building States: mkazo ukiwa katika  ujumuishwaji  katika  mchakato wa  maboresho ya   taasisi za usalama. Inclusivity in secjurity sector reform ( SSR)

katika  ufunguzi huo Balozi Mwinyi aliwaeleza washiriki wa semini hiyo kwamba,  wakati Tanzania  ikiihakikishia  Jumuiya hiyo ya Kimataifa na hususani Umoja wa Mataifa,  wa kuendelea kushirikina nayo katika ujenzi huo wa amani,  bado inaamini na ingependa kusisitiza kwamba     serikali husika ndiyo  inayopaswa kuwa mmiliki na muhusika mkuu wa mchakato  mzima wa uboreshwaji wa taasisi za   usalama .

“ pamoja na  mambo mengine,  ningependa kusisisitza umuhimu wa dhana kuu ya msingi inayosimamia mchakato mzima wa maboresho ya taasisi za  usalama, na dhana hii ni  umiliki wa nchi husika katika   utekelezaji wa mchakato huu” akasisitiza Balozi Mwinyi

 Na kuongeza ,   pamoja na kwamba, serikali husika ndiyo mwenye dhamana  na mmiliki wa mchakato mzima wa SSR,  itakuwa ni jambo jema kama wadau wengine nje ya serikali husika wakashirikishwa au wakajumuishwa katika  majadiliano ya utafutaji wa amani  pamoja na  mchango wa uboreshwaji wa sekta za usalama kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba wadau wote wanakuwa katika muelekeo mmoja ili kuepusha migongano.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushirikiana na Japani katika uaandaji na uendeshaji wa semina za aina hii kabla ya  kuungana na Slovakia.

Pamona na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kushirikia katika ufunguzi wa semina hii, Manaibu wawakilishi wa Japani,  Balozi Kazuyoshi Umemoto na   Balozi Igor Vencel Slovakia nao walizungumza.

Aidha Bw. Dmitry Titov,katibu Mkuu  Msaidizi anayehusika na Masuala ya Utawala wa Sheria katika  Idara ya  Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa  Mataifa Bw. Dmitry Titov
 Naibu  Muwakilishi wa Kudumu wa Japan katika Umoja wa Mataifa,  Balozi, Kazuyoshi Umemoto akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya siku moja
  Balozi Igor Vencel, Naibu Muwakilishi wa Kudumu  wa Slovakia naye akisema machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Washiriki wa  kutoka Balozi mbalimbali,  Umoja wa Mataifa na  Asasi zisizo za kiserikali wakifuatilia hotuba za ufunguzi wa semina  hiyo waliokaa  mstari wa mbele ni watoa mada akiwamo  Bw. Dmitry Titov wa kwanza kulia ambaye ni  Katibu Mkuu Msaidizi anayehusika na  masuala ya utawa wa sheria katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa  Amani  katika Umoja wa Mataifa ( DPKO)

This entry was posted in

Leave a Reply