Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kigoma kuanza ziara ya siku tano mkoani humo jioni hii.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Walid Kaborou akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga na Katikati ya Kinana na Dk. Kaborou ni Mjumbe wa NEC Balozi Ali Karume
Kijana wa UVCCM, Khadija Kanyoye akimvisha skavu Kinana Uwanja wa Ndege wa Kigoma
Kinana akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Kaborou wakati akipita katika paredi la UVCCM wakati alipopokelewa Uwanja wa Ndege wa Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu, Isaa Machibya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alitua Kigoma leo asubuhi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia Nape. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma na Katikati yao ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mjumbe wa NEC, Kirumbe Ng'enda Uwanja wa Ndege wa Kigoma
Kinana akimsalimia Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Stanley Mkandawile, Uwanja wa Ndege wa Kigoma
Kinana akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog