Google PlusRSS FeedEmail

WAJAWAZITO WILAYANI KILWA WAPATA VITANDA VYA UZAZI.

Na Abdulaziz Video

AKINA mama wajawazito katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,wameanza kuondokana na tatizo la kukosa vifaa wakati wa kujifungua,baada ya Halmashauri ya wilaya hiyo kununua vitanda kumi (10) vitakavyotumika kutolea huduma ya kujifungulia. Kununuliwa kwa vitanda hivyo ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete,alilolitoa hivi Mwishoni mwa Mwaka jana alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo zinazotekelezwa katika Mkoa huo ambapo aliiagiza Halmashauri hiyo kununua kitanda baada ya kupokea kero hiyo katika Kata ya Mitole Wilayani Kilwa, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Addoh Mapunda, Akiongea na mtandao Ameeleza   kuwa kununuliwa kwa vitanda hivyo 10 ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais.


Kutokana na agizo la Rais,Halmashauri ya wilaya hiyo Imenunua vitanda zaidi ili kusaidia zahanati kumi kati ya 46 zilizopo ndani ya wilaya hiyo. Zahanati zilizonufaika na mpango huo ni,Mt Kimwaga,Nandembo,Kisangi, Kimbarambara,Kibata,Ngarambe,Tingi na Kanadawale, Jimbo la Kilwa kaskazini, ambapo kwa Jimbo la Kilwa kusini ni,Rushungi,Pande na Mitole.

 Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Hamisi Ulega alikabidhi Kitanda cha Zahanati ya Mitole ambapo wananchi walitoa kero hiyo kwa Rais Sambamba na kununuliwa kwa vitanda hivyo,Halmashauri hiyo pia imenunua seti (12) za kuzalishia ambapo kila seti moja imegharimu kiasi cha Sh,400,000/=

 Nae, Addoh Mapunda,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema kununuliwa kwa vitanda hivyo, sio tu ni utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete, pia ni uendelezaji wa utekelezaji wake, kwani tayari Zahanati 36 kati ya hizo 46 zilikwisha nunuliwa vitanda vya aina hiyo na kufanya Zahanati zote kuondokana na tatizo hilo kwa sasa Ni kweli Zahanati za Kilwa na Jiografia ya kufika Hospital ya Wilaya au Mkoa ni Ngumu sana ila Jitihada za Idara ya Afya,Pamoja na Utawala yaani Ofisi yangu Tukishirikiana na Mkuu wa Wilaya kwa kutafuta Ufadhili Tumeanza kujidhatiti kusaidia Jamii ila Naomba Hata Madiwani Watupe Ushirikiano kwa kuwa wao kwa kushirikiana na watendaji na Wenyeviti wa Vijiji Watasaidia kushauri ili sisi Tujikite katika Uboreshaji wa Huduma kwa Karibu.Alimalizia Mapunda.

Decemba 04 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea Shule ya Sekondari ya kata ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa,katika risala yao wananchi walimuomba kuwasaidia kuwapatia kitanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito,ambapo naye aliuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kutekeleza hilo.


 Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mheshimiwa Abdallah hamis Ulega akiwa pamoja na mkurugenzi na watendaji wengine wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika zoezi la kukabidhi vitanda na seti za kuzalishia kwa hospitali na zahanati zilizopo katika halmashauri hiyo.

Moja ya vitanda ambavyo vimenunuliwa na halmashauri ya mji wa kilwa ili kusaidia akina mama wajawazito.

This entry was posted in

Leave a Reply