Google PlusRSS FeedEmail

KINANA ATEMBELEA SHULE ILIYOKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI CHINA MWAKA 2008

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, akitazama vifaa vya michezo ya watoto katika shule ya  awali ya Kijiji cha Dantong, jimbo la Sichuan, Msafara wa Kinana ambao Amina yumo, ulipotembelea kijiji hicho kuona shughuli za mradi wa kilimo wa kupunguza umasikini, Machi 16, 2013. Kinana yupo China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, na Watatu kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Khadija Aboud. (Picha na Bashir Nkoromo)

Wakulima walipo katika Kijiji kinachoendesha amradi wa kupambana na umasikini wa kilicmo cha Nanchong, jimbo la Sichuan, wakiwa kazini Machi 16, 2013.

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za  kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo)

Shamba la kabichi katika kijiji cha Nanchong, jimbo la Sichaun, China, Shamba hilo lipo katika mradi wa kupunguza umasikini katika kijiji hicho unaofanywa na serikali ya Jimbo la Siachuani ya Chama Cha Kikomunisti cha China. (Picha zote na Bashir Nkoromo.

"KILIMO CHA AINA HII NTAKIPELEKA MKOANI KWANGU", Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema wakati akiwa kando ya shamba la kisasa la njegere, katika kijiji cha Nanchong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Jesca yupo katika msafara wa viongozi 14 wa CCM unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana nchini China.

 Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama moja ya mashamba makubwa ya wakulima walipo kwenye mradi wa kupunguza umasikini, katika Kijiji cha Dantong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).


This entry was posted in

Leave a Reply