Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim
wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali 
za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake Machi 16, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa
katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita  Machi 16, 2013.


Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya  Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo Machi 16, 2013


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam,  Machi 16, 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki  wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam,  Machi 16, 2013


This entry was posted in

Leave a Reply