Google PlusRSS FeedEmail

KINANA ATUA BEIJING, ALAKIWA NA MARMO

"KARIBU BEIJING", Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, baada ya Kinana na ujumbe wake kuwasili akitokea jimbo la Sichuani,Machi 17, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini china kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Balozi wa Tanzania Nchini China, Philip Marmo akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China, baada ya kuwasili  Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai. 

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza, nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Beijing, China, Philip Marmo (wapili kushoto), baada ya kuwasili , Machi 17, 2013 akitokea Sichuan. Kinana na Ujumbe wa viongozi 14 wa CCM yupo nchini China tangu Machi 11, mwaka huu, akiwa katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai na Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mjumbe wa Kamti Kuu ya CCM,  Kadija  Aboud.

Baadhi ya Watanzania waliopo jijini Beijing, China wakichangamkia kupigapicha na Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (Katikati) nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China.

 Baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing, wakilaki Kinana na msafara wake, nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing China,  Machi 17, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing,, Daninga .Daniel.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani akiwasalimia baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing China, baada ya kuwasili na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, nyumbani wa Balozi wa Tanzania nchini China, Philp Marmo, Machi 17, 2013. Kamani ni miongoni mwa viongozi 14, wa CCM waliopo katika msafara wa Kinana ambaye yupo nchini China na ujumbe huo kwa ziara ya Kikazi nchini humo, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China.

This entry was posted in

Leave a Reply