Google PlusRSS FeedEmail

SLAA AMTISHA IGP MWEMA.


  •  Atuma ujumbe, asisitiza kuvunja sheria
  •  Mrema aja juu, CHADEMA inabebwa
  • UVCCM wamshukia  John Tendwa.

Na. Selina Wilson
Vurugu za CHADEMA mikoani zimechukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk . Wilbrod Slaa, kumtumia ujumbe wa vitisho Mkuu wa Jeshi la polisi(IGP),Said Mwema.

Ujumbe huo uliotumwa kwa njia ya simu ya mkononi unamtaka IGP Mwema kuhakikisha askari wanakuwa na mabomu ya machozi, bunduki na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa CHADEMA watakaokuwa wakifanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.

Dr Slaa pia amesema iandaliwe karamu ya mauaji, kwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejipanga kukabiliana na polisi wataksokuwa wakiwadhibiti.

Pia amemueleza IGP Mwema na askari wake wajiandae kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.

Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu vurugu zilizotokea juzi, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten, Daudi Mwangosi.

Chagonja alinukuu ujumbe uliotumwa kwa IGP mwema uliosema “Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague”

Akizungumzia ujumbe huo, Chagonja alisema unaonyesha kiburi,ukaidi na kutotii sheria, hivyo jeshi la polisi litachunguza na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa.

Source; Gazeti la Uhuru. Na. 21287 Jumanne Septemba 4, 2012
 

This entry was posted in

5 Responses so far.

  1. “Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague”

    Mbona huu ujumbe na masimulizi yenu vinapishana sana.. Mkitaka kuwa salama nawashauri msiwe wasemaji wa Jeshi la Polisi ama la Mjitangaze kuwa ni ninyi ndio manosuka mpango wa kuua watanzania.
    Ni ajmabo la kushangaza sana CHADEMA wanafanya vikao vya ndani, wanapigwa na mabomu hadi waandishi kuuwawa wakati huo huo CCM wanafanya mkutano wa hadhara wa mamia ya watu Zanzibar kuzindua kampeni.

    Sidhani kama kuna mtu ana akili njema anaweza kushabikia vitendo vya mauaji ya makusudi vinavyofanywa na Polisi.. na ninyi mnaandika ksihabiki eti vurugu za chadema.. Waacheni wenyewe muone kama kuna hata sisimizi atakanyagwa!!

    La kukumbuka, siku amani ikitoweka mazima hakuna atakaesalimika, hata wewe unaeandika kushabikia udhalimu hutakuwa na pa kutokea!! Askari hawatakaa watokee kuwa na uwezo wa kuwashinda wananchi waliochoka kunyanyswa!!

    Kikwete ataondoka madarakani kwa rekodi ya aina ayeke..kuua raia wasio na hatia kwa makusudi ili tu chama chake kisalimike ...

    Let us count days! As you keep on killing... peole hate you more!!

  2. Kauli anazotoa slaa zinaonyesha wazi kuna watu wako nyuma ya cdm na wamejiandaa na vurugu tunaomba serikali iwemakini

  3. KIYUNGI says:

    Hivi mbona hizi vurugu ni chadema tu kwani wenyewe ni kina nani?

  4. Salma says:

    kwani huyu slaa ni kama nani hadi awe juu ya sheria?

  5. Bwana Mjezi hapo juu, Unajenga au unabomoa? Yaani unaona ni afadhali polisi waandae risasi nyingi ili watu wazidi kufa kuliko Chadema isifanye maandamano? hivi kweli Unaungana na Padre Slaa kuhakikisha mnajaribu kuwasaidikisha Watanzania masikini ya Mungu ambao wengi hawajui maana ya kutekwa kisaikolojia, waamini kwamba Hapa Tanzania wanapata dhiki mno kiasi kwamba bora wafe? Unajua ninyi na baadhi ya watu wa Chadema Kama wewe ana Slaa, ni sawa na mtu anayekwenda dukani kununua sumu ajiue, halafu anadai cheji!!!, Hamuoni taabu kuhamasisha watu waone fahari kufa, halafu wakati huo huo mnajifanya wapenda amani. Jamani hata mkiasi vipi lakini muogopeni Mungu maana YUPO.

Leave a Reply