Google PlusRSS FeedEmail
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waumini wa kanisa la TGMIT lililopo Mwanza, Katibu wa NEC aliwaeleza waumini waliohudhuria ibada hiyo maalumu kuwa amani tuliyokuwa nayo imeletwa na Mwenyezi Mungu hivyo tusiruhusu ipotee.
 Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la TGMIT Florence Ndaki akiongoza ibada maalumu ya kuiombea Tanzania amani, katika ibada hiyo viongozi mbali mbali walialikwa kutoka serikalini ,vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali.
Waimbaji wa Kwaya maarufu nchini Martha Ramadhani na Mary Ruhasha wakiimba wimbo maalum wa kuitakia amani Tanzania kwenye ibada maalumu iliyofanyika leo tar.29 September 2013 kwenye knisa la TGMIT Mwanza.
Waumini wa Kanisa la TGMIT  Mwanza wakiwa kwenye maombi maalum ya kuiombea Tanzania amani, ambapo Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye alikuwa mgeni mwalikwa na viongozi wengine kutoka serikalini,asasi zisizo za kiserikali na vyama vingine vya siasa.

NAPE AHUDHURIA IBADA MAALUMU YA KUIOMBEA AMANI TANZANIA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape ... [Read More]

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecela amesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

 Daktari. Mwelecele Malecela ameiambia Father Kidevu Blog, katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.

"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).

Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 

Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.

IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA 8 TANZANIA

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kur... [Read More]








©2013 CCM Blog

BAADHI YA MAGAZETI LEO SEPTEMBA 26, 2013

©2013 CCM Blog [Read More]

  • AFANYA ZIARA MUSOMA MJINI
  • ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA MAJI
  • ASEMA WANANCHI WANAHAKI YA KUHOJI MAENDELEO YAO
  • AWATAKA WANANCHI KUTAMBUA MASUALA YA MSINGI YANAYOWAHUSU
  • ZAIDI YA VIONGOZI SITA KUTOKA UPINZANI WAJIUNGA CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.

Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA

AFANYA ZIARA MUSOMA MJINI ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA MAJI ASEMA WANANCHI WANAHAKI YA KUHOJI MAENDELEO YAO AWATAKA WANANCHI KUTAMBUA MASUALA Y... [Read More]

Agosti 27, 2013, Chama Cha Mapinduzi kilitoa matamko kadhaa yaliyokuwa yamepitishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa mjini Dodoma. Baadhi ya mambo ambayo CCM kupitia kwa Katibu wake wa NEC, Irikadi na Uenezi Nape Nnauye iliyoyaeleza kwa waandishi wa Habari tena yakiwa yameandikwa kwenye karatasi ambazo baadaye waandishi hao walipewa, Kamati Kuu hiyo vilivyokuwa imelishughulikia suala la madiwani wanane wa CCM waliokuwa wamefukuzwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Miongoni mwa maamuzi waliyopewa waandishi wa habari ni kwamba, Kamati Kuu iliitaka serikali kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seriali (GAC) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo  yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe kwenye Baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za mitaa.

Sasa mdau, soma habari hii hapo chini, kama ilivyoandikwa leo, Septemba 25, 2013,  katika ukurasa wa 6, gazeti la Jamboleo halafu utafakari kama kweli aliyeandika habari hii alielewa vema na kujiridhisha vya kutosha mantiki ya habari yake kabla ya kumpatia mhariri

Zipo hoja nyingi kwenye habari hii lakini MOJA: ni kwamba; Kama CAG anakiri kwamba ukaguzi huo unafanyika kwa ombi maalum lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, sasa hapo huyo CAG amemruka vipi Nape? (ingawa hata aliyekuwa ameagiza serikali kumtuma CAG si Nape ni Kamati Kuu ya CCM, ila Nape alikuwa msemji tu wa agizo).

PILI: Hivi ni hekima ya aina gani inayoweza kusadiki kwamba, agizo au hata ombi linalotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenda kwa CAG, halimhusu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye bosi wa hao wote!

Vifuatavyo ni vipande vya habari hiyo na Press Release ya CCM inayoonyesha kwamba CCM (siyo Nape) iliiagiza serikali yake, kumtuma CAG.




JAMBO LEO, CAG AMEMRUKA VIPI NAPE?

Agosti 27, 2013, Chama Cha Mapinduzi kilitoa matamko kadhaa yaliyokuwa yamepitishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa mjini Dod... [Read More]

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu Obwere wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu Obwere katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati wa uzinduzi wa mradi wa bwawa la maji ya safi ya matumizi ya binadamu na kunyweshea mifugo kata ya Rocha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda nyasi katika (lambo) bwawa la maji linalojengwa katika kata ya Rocha,wilaya ya Rorya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akiwa ameketi pamoja na wajumbe wa shina namba 12 kata ya Utegi tayari kwa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tawi la Nyanduga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Daraja la Asili la Lorbimbe kutoka kwa mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Airo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bukura baada ya kukagua ujenzi wa Maabara,Madarasa na Nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Bukura.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tai kijiji cha Masonga baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Kikundi cha akina Mama  cha Upendo Women Group Masonga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimbeba mmoja ya watoto yatima wanaolelewa na kituo cha  akina mama cha Upendo Women Group.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Hostel ya chuo cha waganga wasaidizi cha RAO HEALTH TRAINING CENTER.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha RAO HEALTH TRAINING CENTER
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa RAO HEALTH TRAINING CENTER ,mwenye kofia ni Mkuu wa chuo hicho Dk. Ziki Makoyo.

MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KATIBU MKUU RORYA

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu Obwere wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nap... [Read More]

  • KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE
  • MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
  • VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
  • WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO

 Mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na mshikamano walio nao.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote za kisheria.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
 Sehemu ya Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba 2013.


CCM YAVUNJA REKODI RORYA

KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISH... [Read More]