Google PlusRSS FeedEmail

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MBARONI KWA RUSHWA

MBEYA, TANZANIA.
KATIBU wa CHADEMA, wilaya ya Mbeya vijijini, James Mpalaza, amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya sh.73,000.

Habari ambazo Daily Nkoromo Blog imezipata, kutoka Mbeya zimesema, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la kata ya Nsalala anatuhumiwa kutenda kosa hilo la kupokea rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata hiyo, Lookred Ndile, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Baraza hilo aliyetajwa kwa jina la Mama Rajabu.

Akithibitisha kukamatwa kwa Katibu huyo wa CHADEMA wilaya, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya, Daniel Mtuka, alisema mtuhumiwa huyo alinaswa na maofisa wa Idara hiyo leo saa 6:00 mchana.

Mtuka alisema kigogo huyo wa CHADEMA, alikamatwa katika ukumbi unaotumika kushauri na kutoa hukumu za kesi zinazofikishwa kwenye Baraza la Kata ya Nsalala, iliyopo wilaya ya Mbeya vijijini.

Kwa mujibu wa Mtuka, TAKUKURU walipokea taarifa kutoka kwa Ndile kuwa viongozi hao wawili wamemuomba rushwa ya shilingi 73,000 ili waweze kumpa nakara ya kesi yake aliyokuwa ameshindwa pamoja na muenendo mzima wa kesi hiyo.

Akifafanua zaidi, Mtuka alisema Ndile alikuwa ameshtakiwa na Monica Degule wakigombania mpaka uliopo kati ya nyumba zao na shauri hil lililopsikilizwa katika Baraza hilo la kata Monica alishinda.

"Baada ya hukumu kutolewa Ndile hakuridhika nayo na hivyo kuandika barua ya kuomba hukumu na muenendo wa kesi ili aweze kwenda ngazi za juu zaidi ambapo alitakiwa kulipa gharama ya shilingi 10,000.

Mtuka aliongeza lakini alipoenda na kiasi hicho ambacho ndiyo kinatakiwa kisheria, watuhumiwa hao wawili walimueleza Ndile kuwa anatakiwa kupeleka shilingi 73,000 ili apatiwe vitu hivyo alivyokuwa anavihitaji.

Alisema ndipo Ndile alipoenda kutoa taarifa TAKUKURU ambapo alipewa kiasi hicho cha fedha na maofisa wa Idara hiyo waliweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili akiwemo Katibu wa CHADEMA wilaya ya Mbeya vijijini.

Naye Ndile akizungumza na Uhuru alisema alihukumiwa kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja, kulipa gharama za Baraza na akishindwa kutekeleza hayo atatakiwa kufyatua matofali 1000 na pia kumlipa Monica gharama zote alizotumia katika kesi hiyo.

"Nilipewa muda wa siku 40 kukata rufani ya kesi yangu na hivyo nikalazimika kuandika barua ya kuomba nakara ya hukumu na mwenendo mzima wa kesi, ambapo awali nilitakiwa kulipia sh.10,000 lakini nilipoenda na kiasi hicho niligeuziwa kibao na kutakiwa kulipa sh.73,000 ndipo nikaenda kutoa taarifa TAKUKURU" alisema Ndile.

This entry was posted in

Leave a Reply