Google PlusRSS FeedEmail

MAAZIDHISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, MKOANI LINDI

Afisa Uraghashi na mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Ndugu Philemona Marijani akitoa maelezo juu ya Banda la WAMA kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Lindi Ndugu Anna Maro katika maazimisho ya Siku ya ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi, Leo Tarehe 01st December 2012.


Wageni mbalimbali pamoja na maafisa wa serikali ngazi mbalimbali mkoa wa Lindi wakiwa mbele ya jengo la WAMA wakisubiri kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda hilo. Katika Maazimisho yaliyofanyika hii leo kitaifa  Mkoani Lindi.


Afisa Uraghishi wa Mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Ndugu Philemona Marijani (wakwanza Kulia) akiwa na Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Taasisi hiyo Ndugu Gloria Minja (wa katikati) na Mwajuma Lubu Muelimishaji wa Taasisi hiyo ya WAMA Mkoani Lindi.   


Wanawake na Wananchi mbalimbali wa Mkoani Lindi wakiwa katika Banda la WAMA kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda hilo, wa kushoto ni Zena Tozo Muelimishaji Afya ya Msingi kwa Jamii kutoka Wilaya ya Bagamoyo ambayo ni mmoja wa waelimishaji Afya wa WAMA katika kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.    


Wananchi mbalimbali wa Mkoani Lindi wakiwa wamepanga foleni katika Banda la WAMA kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda hilo.


Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Ndugu Daud Nassib akiwa anagawa fulana za Taasisi hiyo kwa Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi waliohudhuria katika Maazimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi, leo tarehe 01 Dec 2012.


Vicky Chuwa mmoja wa maafisa wa UNICEF hapa nchini akiwa katika Banda la TACAIDS kwenye maazimisho ya Siku ya Ukimwi iliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi.




Jukwaa Kuu katika Uwanja wa Ilulu likiwa limepambwa tayari kutumika katika Maazimisho hayo.






Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wakiwa wamehudhuria na wengine wakiwa wanaendelea kuhudhuria katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi, ambapo yamefanyika Maazimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ukimwi Duniani.



This entry was posted in

Leave a Reply