NA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU. DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa mno na mauaji ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow yaliyotokea usiku wa kuamkia juzi mjini Mwanza.
Katika salamu za rambirambi alizompelekea Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspeka Jenerali Saidi Mwema, asubuhi ya leo, Jumapili, Oktoba 14, 2012, Rais Kikwete ameagiza jeshi hilo kuhakikisha linachukua hatua za lazima kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji hayo.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ACP Liberatus Barlow kilichotokea usiku wa Ijumaa katika jiji la Mwanza ambako watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumwua ofisa huyo mwandamizi wa Jeshi letu la Polisi.”
“Historia ya ACP Barlow ni historia ya mfano katika utumishi wa umma na hususan katika Jeshi la Polisi. Kwa hakika, Jeshi la Polisi limempoteza kamanda hodari na wananchi waTanzania, hususani wale wa Mkoa wa Mwanza, wamempoteza mlinzi shupavu wa usalama wao na mali zao,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake na kuongeza:
“Nakutumia wewe IGP salamu zangu za rambirambi kufuatia mauaji hayo. Kupitia kwako nalitumia Jeshi zima la Polisi pole zangu kwa kuondokewa na mwenzao na katika mazingira yenye kutia uchungu sana. Aidha, kupitia kwako, naomba uniwasilishie salamu zangu za dhati kwa familia ya ACP Barlow ukiwajulisha kuwa niko nao katika wakati huu mgumu sana. Naungana nao katika kuomboleza kifo cha baba yako na mhimili wa familia yao na katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amen.”
Rais Kikwete pia ametumia nafasi hiyo kulitia moyo Jeshi la Polisi. “Kitendo hiki ni kazi ya watu waoga lakini nawasihi kitendo hicho kisiwakatishe tamaa katika kutekeleza wajibu wenu na kufanya kazi nzuri ambayo mnaendelea kuifanya katika nchi yetu ya kulinda usalama wetu na mali zetu,”
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
October
(36)
- BULEMBO MWENYEKITI MPYA WAZAZI CCM
- VIJANA HAWA WANAHITAJI KUSAIDIWA...
- DR SHEIN AHIMIZA AMANI NA USALAMA ZANZIBAR.
- NAPE , MAIGE NA MGEJA KATIKA KUFUNGA KAMPENI ZA UC...
- MKUTANO WA JUMUIYA YA VIJANA WA CCM, DODOMA LEO.
- UCHAGUZI MKUU UVCCM KUANZA KESHO
- NAPE,CHAMI, MAREALE WAWASHA MOTO KILEMA KUSINI
- HOSPITALI YA HURUMA KUBEBA WAGONJWA KWA PIKIPIKI M...
- NAPE AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA NANJARA RE...
- DR CYRIL AUGUST CHAMI AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA C...
- RAIS AWAAPISHA MJUMBE (MBM),NAIBU MAWAZIRI NA NAIB...
- UNEC-UVCCM KULETA VIJANA WACHAPA KAZI ZAIDI
- KATA YA MSASANI YAPONGEZANA KUKAMILISHA UCHAGUZI S...
- UCHAGUZI MKUU CCM NOV.11
- MADABIDA MWENYEKITI MPYA MKOA WA DAR ES SALAAM
- RAIS KIKWETE ASTUSHWA KUUAWA KWA KAMANDA WA POLISI...
- RAIS AZIMA MWENGE SHINYANGA
- KAMANDA WA POLISI MWANZA AUAWA KWA RISASI
- MTANGAZAJI WA DEUTSCHE WELLE AFRIKA AAGWA RASMI
- TUMUENZI MWALIMU KWA VITENDO
- KATIBU MKUU WA CCM APATA UGENI KUTOKA EU NA DFID
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MFANY...
- TANZANIA YAUKWAA TENA UJUMBE BARAZA LA UTAWALA LA ...
- SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA MSD...
- DK BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KILELE CHA MA...
- MAKALA MAALUM
- RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI LEO
- ASHA ABDALLAH JUMA APETA BARAZA KUU LA UWT
- JIJI LAZIDI KUSAFISHWA
- CCM YAINYONG'ONYESHA CHADEMA ARUSHA
- SUMAYE AWABEZA WANAOMUOTEA KUHAMA CCM
- UTEKELEZAJI WA ILANI YA C C M
- WAJUMBE WA TUME YA KATIBA WAANZA TATHIMINI YA KAZI...
- SHIRIKA LA POSTA NA HADHI YA KIMATAIFA
- WAZIRI HUVISA APATA UGENI
- LOWASSA ASHINDA MONDULI
-
▼
October
(36)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.