Google PlusRSS FeedEmail

SUMAYE AWABEZA WANAOMUOTEA KUHAMA CCM

*Asema hafikirii kuingiwa na ibilisi wa aina hiyo
* Asema hayupo CCM kwa ajili ya madakata

Frederick Sumaye

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Ikiwa ni siku mbili baada ya gazeti la Mwananchi kuandika katika ukurasa wa kwanza habari iliyoambana na picha ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, 'likiuza' kwamba Sumaye ateta na Chadema kuhusu hatima yake kisiasa, leo Waziri Mkuu huyo mstaafu amesema hawezi kuhama CCM.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, ndoto za wanaodhani kwamba atahama CCM kwenda chama kingine, ni sawa na fisi anayevizia mkono wa mtu akidhani utakatika lakini asiambulie kitu.

"Napenda kueleza wazi kwamba, sina nia wala ndoto ya kuhama CCM kwenda Chama chochote, mimi sipo CCM kwa sababu ya cheo", alisema Sumaye.

Akizungumzia kushindwa kwake ujumbe wa NEC katika uchaguzi wa Hanang, Sumaye amedai rushwa imesababisha kuanguka kwake.

Katika uchaguzi huo, ambao ni miongozi mwa chaguzi za CCM zinazoendelea nchini kote katika nafasi mbalimbali, Mary  Nagu aliibuka mshindi.

This entry was posted in

Leave a Reply