Google PlusRSS FeedEmail


Wageni wlikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa. 6a 
Seraphin Lusala Mkurugezni wa Masoko na Mauzo Serena Hotel kulia akiwa katika hafla hiyo. 9a 
Msanii Wanne Star kushoto na kundi lake wakitoa burudani katika hafla hiyo. 13a 
Burudani kutoka kundi la Wanne Star ikiendelea wakati wa hafla hiyo 14a 
Meneja wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena Katikati, Emmanuel Okware Meneja wa mauzo kutoka Quatar Airways kulia na mdau Juma Mabakila wakiwa katika hafla hiyo. 15a 
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo 18a 
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo 20a 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na maofiza wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.
................................................................................................
(HOTUBA YA MH. WAZIRI RAZALO NYALANDU WAKATI WA UZINDUZI WA SITE)
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote mliofika katika tukio hili muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa kwa onesho jipya la utalii la kimataifa litakalojulikana kwa jina la Swahili International Tourism Expo (S!TE).
1. Sekta ya Utalii ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa kwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile usafirishaji, viwanda na biashara, kilimo, sanaa za mikono na kadhalika. Sekta ya utalii ina uwezo wa kuongeza ajira kwa haraka zaidi na inatambulika kwamba kila mtalii mmoja anapokuwa nchini huchangia takribani nafasi 12 za ajira za aina mbalimbali. Aidha, Utalii ni tasnia muhimu katika kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza mahusiano ya kijamii na vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya kihistoria na maliasili. Hapa nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka 2002 na 2013, utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%, kutoka watalii 575,000 mwaka 2002 wambao waliliingizia taifa Dola za Marekani milioni 730 hadi kufikia watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao waliingizia taifa Dola za marekani Bilioni 1.81.
2. Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya maliasili na utamaduni vya kipekee. Kutokana na kuwepo kwa vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya World Economic Forum katika taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya Utalii (Travel and Tourism) imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) duniani ikiongozwa na Brazili kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi asilia wa kimataifa, wingi wa wanyamapori na ardhi kubwa iliyo hifadhiwa. Hakika, ni ukweli usiopingika kwamba katika vivutio saba vya maajabu ya asili katika bara la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni ushuhuda kwamba juhudi zetu za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda. Hivi sasa Bonde la Ngorongoro; hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima Kilimanjaro ni vivutio ambavyo vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya asilia barani Africa.
3. Hata hivyo, hatuwezi kutegemea tu uwingi na ubora wa vivutio hivi vya utalii peke yake. Ni muhimu kuongeza juhudi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili kujenga uelewa wa utajiri huu kidunia. Kama taifa, tunahitaji juhudi na mikakati zaidi ili kutangaza vivutio vyetu.
4. Kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea kutangaza utalii wetu na kuifaya Tanzania iweze kushindana kimataifa, mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), iliingia makubaliano na kampuni inayojulikana kama Pure Grit Project and Exhibition Management LTD, hapo mwanzo ilijukana kama Witch & Wizard Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa nchini Tanzania yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo -S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi Oktoba, 2014. Pure Grit Project and Exhibition Management LTD ni kampuni inayoendesha maonesho ya utalii ya INDABA ambayo ni maonesho ya tatu kwa ukubwa duniani. Onesho la S!TE litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi Oktoba kila mwaka katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na kujikita zaidi katika kuvutia washiriki kutoka ndani nan je ya nchi.
5. Mkoa wa Dar es Salaam umechaguliwa mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa onesho la S!TE kutokana na sehemu ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo wa miundombinu bora na huduma nzuri zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa.
6. Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho hili ni kama ifuatavyo.
6.1 Mwenendo wa idadi ya washiriki hadi sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya nafasi za maonesho hayo tayari zimejazwa kwa kuchuliwa na makampuni binafsi na Bodi za Utalii za nchi mbalimbali. Aidha, kuna idadi kubwa na ya kuridhisha ya maombi ya washiriki inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni kwamba ifikapo katikati ya mwezi Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia asilimia 100.
6.2 Programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii: Katika kuhakikisha kuwa onesho hili linakuwa ni fursa ya kuwaunganisha wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania na masoko ya Utalii, S!TE itakuwa na programu maalum (Hosted buyer and travel writer programme) ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii na waandishi wa habari za utalii (Tour Operators, Wholesalers, Packagers and Travel Agents and Travel Writers) na kuwapangia ratiba maalum ya kuonana na washiriki wa maonesho hayo ili kuwawezesha kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Mawakala hao wapatao ishirini na wandishi wa habari kumi watagharimiwa (hosted) na S!TE.Hadi kufikia Juni 2014,mawakala 13 kutoka Marekani, Australia, Ujerumani, Uholanzi, India, Mexico, Norway na China wamethibitisha ushiriki wao.
6.3 Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho la S!TE lina tovuti ijulikanayo kama www.site.co.tz. Tovuti hii imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya onesho lenyewe ambapo inataarifa nyingi zinazoweza kumfanya yeyote anayetembelea tovuti hiyo kupata taarifa zote muhimu kwa muda mfupi. Kwa mfano tovuti inatoa taarifa za ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho yatayojengwa na kumruhusu mteja kuchagua eneo kulingana na uwezo wake. Aidha, tovuti hii ambayo pia imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook, inapatikana kwa lugha mbalimbali
7. Pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, S!TE ina lengo la kuunganisha wafanya biashara wa Utalii wadogo na wa kati wa Tanzania (Small and Medium Tourism Enterprises - SME’s), na masoko ya utalii ya kimataifa. Ni ukweli kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo mdogo wa kimtaji wa kuweza kufikia masoko ya utalii ya kimataifa. Kupitia S!TE, hasa kupitia programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii, itasaidia katika kutatua changamoto hii.
Naomba watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii nchini.

WAZIRI WA MALISILI NA UTALII AZINDUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO (SITE)

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akipongezana na Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii... [Read More]

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimpatia  mkazi wa Zanzibar, Badrudin Alidina tiketi ya ndege  na vibali vya kwenda kufanya kazi ya udereva Dubai, Falme za Kiarabu,  katika hafla iliyofanyika Keko jijini Dar es Salaam ambapo pia wanawake watano walipatiwa tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi  mbalimbali Qatar Uarabuni.
Dereva,  Maneno Tamba akipokea tiketi na vibali hivyo kutoka kwa Mtemvu
 Hamud Ramadhan akipokea tiketi na vibali vya safari kwenda kufanya kazi ya udereva Dubai
Dereva Salum Rashid akikabidhiwa tiketi na vibali kwa ajili ya safari hiyo
 Dereva, Khatib Mohamed Waziri akikabidhiwa na Mtemvu  tiketi na vibali  kufanya kazi ya udereva Dubai.
 Mkazi wa Dar es Salaam, Rahma Salehe akipokea tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi Qatar, Falme za kiarabu
Mkazi wa Dar es Salaam, Hindu Khamis akipokea tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi Qatar, Falme za kiarabu

BRAVO JOB CENTRE YAPELEKA VIJANA KUMI KUFANYA KAZI DUBAI, WATANO NI WA TRIP YA KWANZA YA MADEREVA

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimpatia  mkazi wa Zanzibar, Badrudin Alidina ti... [Read More]


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) ( Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria).

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATAALAMU WATATU WA UTAFITI WA CHANJO YA MALARIA KUTOKA IFAKARA HEALTH INSTITUTE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (I... [Read More]

Matokeo ya Mtihani wa Majaribio (Mock) kwa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu na Kidato cha Sita mwakani, yatachangia alama 10 za Alama Edelevu (CA).
Kwa utaratibu huu, matokeo ya mwisho ya mtahiniwa, yatatokana na asilimia 30 ya Alama Endelevu na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa.
Asilimia 30 za Alama Endelevu, zitapatikana kutokana na mitihani mbalimbali.

Kwa Kidato cha Nne mwaka huu, alama hizo zitatokana na matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambao utakuwa na alama 10, matokeo ya kidato cha tatu muhula wa kwanza na wa pili alama tano, matokeo ya mtihani wa majaribio (mock) wa Kidato cha Nne ni alama 10 na majaribio ya kazi alama tano.

Utaratibu huu umetokana na viwango vipya vya ufaulu, vilivyoainishwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwenye kitabu cha Mwongozo wa Matumizi ya Viwango vya Ufaulu na utaratibu wa kutunuku matokeo ya kidato cha nne na sita.
Kwa Kidato cha Sita, zitatokana na matokeo ya mtihani wa Kidato cha Tano muhula wa kwanza na pili alama 15, matokeo ya 'mock' alama 10 na kazi mradi itakuwa ni alama tano.
“Katika somo ambalo mtahiniwa hakufanyia Kazi za majaribio, alama za matokeo ya Mitihani ya 'Mock' ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, itachangia alama 15 badala ya 10 zilizoainishwa,” imefafanua sehemu ya mwongozo huo.

Katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana na Kidato cha Sita mwaka huu, mchanganuo wa alama 30 za Alama Endelevu ni alama 15 zinazotokana na matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, asilimia 10 ilitokana na maendeleo ya mitihani ya kidato cha Tatu muhula wa Kwanza na Pili na matokeo ya muhula wa Kwanza Kidato cha Nne na kazi za majaribio asilimia tano.
Kwa Kidato cha Sita, alama endelevu ni matokeo ya Kidato cha Tano kwa mihula yote miwili ni alama 15, muhula wa kwanza wa Kidato cha Sita ni asilimia 10 na kazi za majaribio ni asilimia tano.
Aidha, Baraza limebadili utaratibu wa kupanga madaraja ya kufaulu, kutoka mfumo wa Pointi na kuwa wa Wastani wa Alama za Mtahiniwa (GPA).
 
Mfumo unaotumiwa sasa wa pointi, huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa kwa masomo aliyofaulu zaidi, na kupanga madaraja kuanzia la kwanza hadi la nne.
Madaraja ya mfumo wa GPA, hupangwa katika utaratibu wa Distinction, Merit, Pass na Fail. Daraja la Distinction ni la ufaulu wa juu zaidi na daraja Pass ni ufaulu wa chini.
Mtahiniwa hutunukiwa madaraja A, B+, B, C, D, E au F kutegemeana na ufaulu wake katika somo ambapo uzito wa alama katika madaraja A = 5, B+= 4, B = 3, C=2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.
Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo, endapo atapata Daraja D ambayo ni sawa na uzito wa alama moja. Ukokotoaji wa jumla ya GPA ya mtahiniwa hufanyika kwa kuzingatia masomo, ambayo mtahiniwa amefaulu angalau kwa daraja D na kuendelea (D, C, B, B+ na A).
GPA anayopata mtahiniwa hutokana na wastani wa pointi alizopata katika masomo saba aliyofanya vizuri zaidi kwa Mtihani wa Kidato cha Nne au masomo matatu ya mchepuo kwa Mtihani wa Kidato cha Sita.
Aidha, GPA ya mtahiniwa huandikwa katika nafasi moja ya desimali ambapo nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi yaliyokaribu.
Mfano, mtahiniwa mwenye GPA ya 3.15 itakuwa sawa na 3.2 na mtahiniwa mwenye GPA ya 3.14 itakuwa sawa na 3.1.
Muundo wa madaraja ya GPA kwa kidato cha nne, Distinction ni 3.6-5.0, Merit 2.6 -3.5, Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5, Fail 0.0-0.2 wakati Kidato cha sita ni Distinction 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass 0.7-1.6, Fail 0.0-0.6

BARAZA LA MITIHANI LAPANGUA MFUMO MZIMA WA KUPANGA MADARAJA YA UFAULU KIDATO CHA NNE NA SITA 2016.

Matokeo ya Mtihani wa Majaribio (Mock) kwa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu na Kidato cha Sita mwakani, yatachangia alama 10 za Alama E... [Read More]

NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
BUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.

Amesema, uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.

Mtemvu amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo, mjini Dar es Salaam.

"Wapinzani baada ya kuona kuwa hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona wanavyotapatapa, mara eti huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia kwenye chaguzi, kuweka mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini hata wafanyeje CCM itawabwaga tu", alisema Mtemvu.

Mtemvu alisema, pale ambapo wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au udiwani ni pale ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.

"Ikifika acheni mambo ya kuanza mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi ambayo husababishwa na baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka wagombea kwa lazima, tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani hawapati hata kiti kimoja cha cha mtaa", alisema Mtemvu.

Mtemvu aliwataka wana-CCM pia kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka nafasi ambao wana fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi kuwa wagombea kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.

Aliwataka mtu anapowajia kwa fedha kuzipokea na kuzila, lakini wakati waanapofikia maamuzi muhimu kwenye uchaguzi wahakikishe wanachagua yule wanayemfahamu kwa thati kwamba anao uwezo wa uongozi.

Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana fedha, hivyo watu wa aina hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.

Mtemvu alisema kiongozi mwenye uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote yupo na watu na anajali maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni wake tu.

"Mfano ni kama hivi tunavyofanya sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara tunapigania wanyonge, juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe hovyo, japo baadhi ya watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti nina maslahi binafsi, khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu kama siyo uzushi ni nini?" alisema Mtevu.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo- CCM Blog

MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA CCM ITAWABWAGA, AWASHANGAA WANAOMSEMA KUWA ANA MASLAHI BINAFSI KUTETEA MAMALISHE TEMEKE

NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE BUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi ... [Read More]

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam. Mtemvu amewapa pole walipoteza mali zao kutokana na moto huo ambao chanzo cha ke hakijajulikana.  Hadi inakisiwa imepatikana hasara ya zaidi ya sh. milioni 97.
 Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
 Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
 Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA KEKO, ATOA POLE

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika ... [Read More]



 

1Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo asubuhi hii wakati wa seina inayojadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio ya mfuko huo, malengo na Changamoto zake katika kufanikisha huduma ya afya kwa jamii, ambapo uwigo wa walengwa katika huduma hizo umeongezeka kutoka kaya 120 mwaka 2009 na kufikia kaya 668.474 mwaka 2014 sawa na wanufaika milioni 4.01 na mpaka sasa mfuko huo unafanya kazi na Halmashauri za wilaya 129 katika nchi nzima kati ya Halmashauri 168 zilizopo lakini pia tayari Halmashauri 20 kati ya hizo zimeshahamasishwa na zitaingia katika mpango huo siyo muda mrefu, .(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-BAGAMOYO) 2Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji akitoa mada katika semina hiyo juu ya uchangiaji wa huduma za mfuko wa bima ya afya kulia ni Raphael Mwamoto Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti na katikati ni Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF) 3Dk Frank Lekey Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Kitaaluma akitoa mada kuhusu uboreshaji wa huduma za mfuko wa Afya ya jamii ambapo kwa sasa wanafanya kazi na hospitali za serikali na baadhi ya hospitali za mashirika ya dini. 4Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF) akizungumzia mafanikio yaliyokwishapatikana kutokana na huduma za mfuko wa Afya ya jamii 5John Bwire Mkurugenzi wa kampuni ya Raia Mwema na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbalzinazotolewa katika semina hiyo 6Kulia ni Mhariri Dany Mwaijega na wenzake wakifuatilia majadiliano ya semina hiyo 7 8 9 10Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri mtendaji wa New Habari Bw. Absalom Kibanda akizungumza katika semina hiyo inayofanyika mjini Bagamoyo anayefuata ni Abdalla Majura kutoka ABM Radio. 11Mhariri wa Gazeti la Mawio Jabir Idrissa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano katika semina hiyo 12Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee na viongozi wengine wa mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi mjini Bagamoyo. 13Wahariri mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kufungua semina hiyo 14Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi na Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wakiwa katika picha ya pamoja. 15Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi katikati ni Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma na Anna Mziray Meneja wa Msoko na elimu kwa umma wakiwa katika picha ya pamoja.

NHIF YATETA NA WAHARIRI MJINI BAGAMOYO

  Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya ... [Read More]


 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkandarasi wa kisima hicho, Onesmo Sigala (wa pili kulia) wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MO Resources Limited,na Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana ( wa pili kushoto).
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ukandarasi ya MO Resources Limited, Onesmo Sigala (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi.

TBL KUWAJENGEA KISIMA CHA MAJI CHA SH MIL. 29 WANANCHI WA SARANGA, DAR

 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi... [Read More]