Na Mwandishi Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, jana alhamisi amezindua rasmi mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) wakati wa mkutano unaohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati 20 wafanyabishara, mashirika ya kimataifa yakiwamo ya fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ambao ni ulioanza Juni 4 na utamalizika Juni 6, unaongozwa na Waziri wa Nishani na Madini Professor Sospeter Muhongo ( Mb) ambaye pamoja na kuhudhuria na kuchangia mijadala mbalimbali, ijumaa ( June 6), atazungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Akizindua mwongo huo Ban ki Moon, pamoja na mambo mengine alieleza kuwa licha ya kuwa pamoja suala la Nishati ni suala la kidunia, lakini katika maeneo mengi ni suala linalomhusu mwanamke zaidi.
“ Ni suala linalomhusu mwanamke zaidi, linaweza kumaanisha tofauti kati ya usalama na hofu, uhuru na utumwa , hata uhai na kifo. Dunia lazima ije pamoja kumaliza umaskini wa nishati na kuhakikisha watu maskini wanaweza kuhimili maisha yao na kustawi kiuchumi” akasema Katibu Mkuu.
Akaongeza kuwa mpango wa nishati endelevu kwa wote zimeanza kuzaa matunda na kwamba ahadi za mabilioni ya dola zilizoahidiwa zimetolewa. Huku nchi zinazoendelea zaidi ya 80 zimejiunga na mpango huo.
Pamoja na Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kuzungumza wakati wa uzinduzi wa mwongo huo, wengine waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Rais wa Iceland, Olafur Ragnar Grimsson, Bw. John Ashe,Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Rais wa Banki ya Dunia Jim Yong Kim ( kupitia video) .
Mkutano huu utafanya tathmini ya matokeo ahadi za mabilioni ya dola kuhusu upatiakani wa nishati, ufanisi wake na nishati mbadala zilizoahidiwa wafanyabiashara, wawekezaji na watu wengine walizotoa wakati wa Mkutano wa Maendeleo Endelevu ( Rio+20) uliofanyika mwaka 2012.
Aidha unatarajiwa kuhamasisha upatikanaji wa raslimali fedha, uwezeshaji na mipango ya kufikia malengo ya nishati endelevu kwa wote.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo Sospeter Muhongo (kulia), akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi (kushoti), wakati wa uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote. Walioketi nyuma ni wasaizidi wa Waziri.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote (2014-2024), uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote ( SE4ALL)unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1000. Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2014
(556)
-
▼
June
(94)
- WAZIRI WA MALISILI NA UTALII AZINDUA MAONYESHO YA ...
- BRAVO JOB CENTRE YAPELEKA VIJANA KUMI KUFANYA KAZI...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATAALAMU WATATU WA UTAFIT...
- BARAZA LA MITIHANI LAPANGUA MFUMO MZIMA WA KUPANGA...
- MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA CCM ITAWABWAGA, ...
- MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA KEKO, ATOA POLE
- NHIF YATETA NA WAHARIRI MJINI BAGAMOYO
- TBL KUWAJENGEA KISIMA CHA MAJI CHA SH MIL. 29 WANA...
- CHADEMA KWAWAKA, WAJUMBE WAKE WA BARAZA KUU NA WAN...
- NATIONAL CONSULTATION FOR LOCALIZATION OF THE POST...
- Katika "HUYU NA YULE" ya NJE-NDANI wiki hii......
- FILAMU YA ESPINHO DA ROSA “THE THORN OF THE ROSE” ...
- RAIS KIKWETE ATUA MALABO, EQUTORIAL GUINEA, KUHUDH...
- DAR ES SALAAM KUWA KIVUTIO KIKUBWA CHA WAWEKEZAJI ...
- MANISPAA YA ILALA YASAINI MKATABA WA BILIONI 2.1 K...
- TANZANIA YATAKIWA KUTENGENEZA AJIRA ZA KUTOSHA
- MAKAMAU MWENYEKITI WA CCM TAIFA AFANYA MAZUNGUMZO ...
- MWELEKEO WA HALI YA JOTO NA MVUA KATIKA KIPINDI CH...
- BAGAMOYO HISTORICAL MARATHON 2014 YAWA KIVUTIO
- TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU, MKUTANO MKUU NA ...
- MAHOJIANO YA KWANZA PRODUCTION NA MKURUGENZI WA MB...
- MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU ASHIRIKI UJENZI OFIS...
- NAPE AWATAKA WASOMI KUSHAURI KATIKA KUBORESHA SERA...
- WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUH...
- ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOY...
- ABBAS MTEMVU ACHARUKA MAMALISHE KUTIMULIWA BILA UT...
- MEYA WA ILALA MH JERRY SILAA ATEMBELEA NA KUKAGUA ...
- RAS INNOCENT NGANYAGWA AKONGA NYOYO ZA WANZIBARI T...
- STAMICO YAAHIDI NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI
- RAIS KIKWETE AKUSUDIA KUSHUKA CHAKI TENA
- WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHIRIKI MAONYESHO ...
- TFF YAJITOSA NA `PLAN INTERNATIONAL` KUTETEA HAKI ...
- MAREHEMU KAHURANANGA KUZIKWA KESHO IJUMAA, DAR ES ...
- MASHINDANO YA NGALAWA YANOGESHA TAMASHA LA 17 LA Z...
- WOMEN WITH ATTITUDE:SINEMA YENYE LADHA YA SHUGHULI...
- VUAI AUPONGEZA UONGOZI WA TAWI LA CCM DMV MAREKANI...
- JAPAN YATOA SH. BILIONI 24 KUSAIDIA BAJETI YA SERI...
- TAARIFA KWA UMMA: ONYO KUHUSU UTAPELI WA AJIRA KAT...
- MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA OFISI Y...
- USILIKOSE COCKTAIL PARTY HILI LA MAANA MJINI
- CHAP CHAP 'JIPIGE MWENYEWE'
- MAHOJIANO YA MOJA KWA MOJA NA MSANII ANNA MWALAGHO...
- ZIARA YA NHC NA WAKURUGENZI WA BODI SINGAPORE
- NAPE ALITEKA JIMBO LA UBUNGO ENEO LA KIMARA
- MHESHIMIWA JENISTA MUHAGAMA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZ...
- HAKIKISHENI TUNAKUWA NA CHAKULA CHA KUTOSHA DKT. B...
- UN KUZINDUA MFUMO MPYA WA KUHABARISHA UMMA NDANI Y...
- BUNGE VS NMB-DODOMA WALIVYOTOANA JASHO(MPIRA WA MI...
- SAUTI SOL WATIKISA TAMASHA LA ZIFF 2014
- MAHOJIANO YA KWANZA PRODUCTION NA FABIAN LWAMBA WA...
- HACKERS WAIBA AKAUNTI YA FACEBOOK YA MEYA WA ILALA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MAADHIMISHO YA...
- BALOZI SEIF IDD ABARIKI TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014...
- VIONGOZI WA CCM WILAYA YA LUDEWA WATAKIWA KUSHIKAMANA
- NAPE ALIPOHUTUBIA WANA CCM WA TAWI LA SAUT KAMBARA...
- TAMASHA LA "NAIAMINIA-TANZANIA" DODOMA
- DEO FILIKUNJOMBE AANDAA SEMINA KWA VIONGOZI WA CCM...
- SHAMRA SHAMRA ZA UFUNGUZI WA ZIFF 2014 NDANI NGOME...
- MINING COMPANIES ARE NOT TAX CHEATS
- NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO USIKU HUU, MWANANYALA A,...
- MTEMVU ATOA MISAADA YA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA ...
- NHC YAVUTIA WAWEKEZAJI MAONYESHO YA NYUMBA DUBAI, ...
- WAZIRI: TUWAEPUSHE VIJANA WETU NA UHAFIDHINA
- SOKO LA MACHINGA KARUME LATEKETEA KWA MOTO
- RAIS KIKWETE ATEUA MANAIBU BALOZI WAWILI
- TRL YASIMAMISHA KWA MUDA HUDUMA ZA USAFURI WA TREN...
- MWENYEKITI WA CHADEMA AHAMIA CCM IRINGA
- MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE TAMASHA LA K...
- DK. ASHA-ROSE: HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA WA SHER...
- TWAWEZA YATUNUKU TUZO WAANDISHI 37 KWA MAONI YAO K...
- JUMUIYA YA WAZAZI (CCM) WILAYA YA ILALA WAIPONGEZA...
- INDIAN FOOD FESTIVAL
- DK. ASHA-ROSE MIGIRO ATINGA KWA KISHINDO OFISI ZA ...
- BALOZI MPYA WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA MAKAMU ...
- RAIS KIKWETE AHANI MISIBA YA KANALI MSTAAFU ALI MW...
- KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKUTANA NA BALOZI WA UI...
- AJALI YA GARI KIBAIGWA, MWIGULI ASAIDIA KUOKOA
- MBUNGE WA MKULANGA AMWAGA MSAADA KWA WAJASILIAMALI
- KASI YA NAPE YAMPATA RAIS WA WANAFUNZI SAUT PAMOJA...
- NAPE APOKELEWA KISHUJAA NA WANACHAMA WA CCM SAUT M...
- VIONGOZI WA TAWI LA CCM SAUT MWANZA WATATHMINI MIA...
- WASOMI WATAKIWA KUCHANGIA MAWAZO YAO KATIKA KUKUZA...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO...
- RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA M...
- BAN KI MOON AZINDUA MWONGO WA NISHATI KWA WOTE (20...
- KINANA ASHUHUDIA MCHIMBAJI MDOGO WA TANZANITE ANAV...
- CHRISTOPHER OLE SENDEKA AKIHUTUBIA WAKAZI WA MERER...
- TAASISI YA FARIDA FOUNDATION KUFANYA UZINDUZI SIKU...
- KINANA AITEKA MERERANI KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
- MWILI WA MAMA YAKE ZITO KABWE WASAFIRISHWA KWENDA ...
- OLE SENDEKA: WANANCHI WA SIMANJIRO KULINDA ARDHI Y...
- MAMA MZAZI WA ZITTO KABWE AFARIKI DUNIA
- KINANA AWASILI WILAYA YA SIMANJIRO
- SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJEN...
-
▼
June
(94)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.