Google PlusRSS FeedEmail

MTEMVU ATOA MISAADA YA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA KWA MIRADI YA MAENDELEO YA JAMII NA VIKUNDI TEMEKE

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (AM)  akimkabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa Umoj wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Kilakala Hashim Swedi (wapili kulia), alipotoa jozi nane za jezi hizo na mipira minane kwa ajili ya timu za vijana kwenye kata hiyo leo, katika hafa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mtemvu ametoa vifaa hivyo kutimiza ahadi aliyotoa alipofanya ziara kwenye kata hiyo siku kadhaa zilizopita.
 Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kilakala, Hashim Swedi akishukuru baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na Mtemvu
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akikabidhi sh. milioni 1.5 kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtoni jimboni humo, Omry Mateso (kulia), katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, leo. Fedha hizo ni kwa ajili ya kuendeleza ujezi wa jengo la Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo.  Katika hafla hiyo zaidi ya vikundi 25 vilipatiwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii au vikundi vya wajasiriamali.
 Mtemvu akikabidhi sh. milioni moja, kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko B, Paulo Milanzi kwa ajili ya fedha hizo kusaidia mradi wa kutandaza mabomba ya maji kwenda kwenye nyumba za wananchi katika mtaa huo.
Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mitaa na vikundi vya wajasiriamali aliowapatia fedha kwa ajili ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya jamii. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply