Jukwaa litakalotumika kwa masuala ya burudani kuanzia leo Juni 14 hadi 22 ndani ya Ngome Kongwe katika ukumbi wa Mambo Club linavyoonekana muda huu kwenye hatua ya mwisho kuelekea ufunguzi rasmi saa moja jioni.(Picha na Zainul Mzige modewjiblog)
Opening Night: Mandela: Long Walk to Freedom
June 14th 20:20 Old Fort Ampitheatre
Opening Night Concert:
June 14th Mambo Club
Tamaduni Music (Tanzania) followed by BODY, MIND & SOUL (Malawi)
Sehemu maalum itakayokuwa ikitoa huduma wa chakula na vinywaji.
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (mwenye t-shirt ya blue) akiongoza baadhi ya wasanii kuelekea jukwaani kwa ajili ya mkutano mfupi na waandishi wa habari waliowasili mchana huu.
Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa “Has T” akiwatambulisha wasanii watakaotoa burudani leo kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi ZIFF kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari (hawapo pichani).
DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto Rico(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna atakavyosugua sahani za muziki usiku wa leo. Wengine ni wanamuziki wa kundi la BODY, MIND & SOUL kutoka Malawi.
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwatambulisha wasanii watakaotoa burudani kwenye ufunguzi wa tamasha hilo.
Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa “Has T”, Andrew Chale kutoka Tanzania Daima, Festo Polea kutoka Mtanzania pamoja na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala wasikiliza vionjo kutoka kwa wasanii wakati wa utambulisho.
Picha ya pamoja na Ma-DJ's na wasanii watakaotoa burudani leo kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014.
Wasanii wa kundi la BODY, MIND & SOUL kutoka nchini Malawi wakiwa na mmoja wa wapiga picha wa ZIFF (katikati).
Ma DJ's watakaotoa burudani siku zote za tamasha la ZIFF 2014.
Wasanii wa muziki wa HIP HOP kutoka kundi la TAMADUNI MUSIC nao watakinukisha usiku wa leo.
Lango kuu la kuingia Ngome Kongwe patakapofanyika tamasha la ZIFF 2014 linavyoonekana muda huu.