Baadhi ya watoto wa shule za msingi jijini Dar wakifanya mazoezi ya maigizo kwa ajili ya tamasha la kesho kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Na Mwandishi wetu
WANAFUNZI wa shule za Msingi nchini, wameshauriwa kuwa na mazoea ya kusoma vitabu kwa lengo la kuwa wagunduzi wa vitu mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Soma, Demere Kitunga wakati wa maandalizi ya tamasha la kwanza la vitabu vya hadithi kwa watoto wa Shule za msingi.
Kitunga amesema kuwa tamasha hilo ni moja ya michakato ya kuwataka watoto kupenda kusoma vitabu hasa vitabu vya hadithi kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.
"Ugunduzi wa jambo fulani unaanzia katika kusoma hivyo watoto wakiwa wanania ya kusoma vitabu mbalimbali hususani vya hadithi wataweza kuongeza uwelewa fulani katika fikra zao,"amesema Kitunga
Aidha amesema kuwa tamasha hilo linatarajia kuanza kesho hadi juni 14 mwaka huu katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini ,ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mmoja wa watoto akionyesha kipaji chake wakati wa mazoezi kwa vitendo kupitia hadithi mbalimbali walizosoma kutoka kwenye vitabu.
Kitunga amesema kuwa Taasisi hiyo hadi sasa imeweza kusambaza vitabu katika Shule mbalimbali za Msingi pamoja na klabu za kujisomea zikiwemo Kurasini ,maktaba pamoja na Chang'ombe.
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na maigizo ambayo yatafanywa kwa kutumia hadithi zilizokuwa katika vitabu hii yote kwa lengo la kukuza utamaduni wa watoto kusoma vitabu.