KINANA ASHUHUDIA MCHIMBAJI MDOGO WA TANZANITE ANAVYOSAIDIA WENZAKE KWA KUWAUZIA KWA BEI NAFUU VIFAA VYA UCHIMBAJI MADINI HAYO MERERANI
Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite kwenye machimbo ya Mererani wilayani Simanjiro, Mahmoud Karia (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahmahn Kinana vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini hayo, ambavyo huviuza kwa wachimbaji wengine kwa gharama nafuu. Karia alipata fursa ya kuonyesha vifaa hivyo Kinana alipomtembelea kwenye eneo la machimbo la mchimbaji huyo mdogo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi mkoani Manyara, mapema wiki hii. Wapili kushoto ni Mbunge wa Simnanjiro, Christopher Ole Sendeka na anayerekebisha miwani ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. (Picha na Bashir Nkoromo- CCM Blog)