Google PlusRSS FeedEmail

CHADEMA MWANZA SASA WATISHANA KUNG'OANA

MWANZA, TANZANIA
Baada ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA wilayani Ilemela, kuupiga ‘stop’ uongozi wake wa wilaya, sasa unatishia kuwang’oa madiwani wake saba, wanaodaiwa kushindwa kulinda kiti cha Meya wa jiji la Mwanza.

Madiwani hao wanadaiwa kukisariti chama hicho kwa kuongoza harakati za kumng’o aliyekuwa Meya wa jiji hilo , Jacton Manyerere, mwezi uliopita baada ya kuungana na madiwani wa vyama vingine kumpigia kura za kutokuwa na imani naye.

Habari zilizopatikana hapa kutoka ndani ya Chadema zimetonya  kuwa, Mkutano Mkuu wa wilaya ya Ilemela, uliofanyika Agosti 12 mwaka huu katika hoteli ya PK wilayani humo, ‘uliwaka moto’ baada ya kuibua hoja ya kutokuwa na imani na viongozi wa mkoa pia madiwani hao.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajumbe na viongozi wapya wa wilaya hiyo watatoana macho na uongozi wa mkoa ambao unadaiwa kutafuna fedha za ruzuku zilizotolewa mkoani Mwanza.

Imedaiwa kwamba, moja ya mambo yaliyohojiwa katika mkutano huo na kusababisha uwake ‘moto’ ni pamoja na ruzuku hiyo, ambayo Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, Wilson Mushumbusi ameshindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi yake katika vikao husika.

“Hadi kieleweke vinginevyo tutatona macho kama mapato na matumizi ya ruzuku hayataeleweka.” Kilisema chanzo kimoja kutoka ndani ya uongozi wa wilaya hiyo na kudai kuwa wajumbe wengi wa kikao hicho wanataka Madiwani hao wakiwemo wawili wa Viti Maalum, walioshindwa kulinda kiti cha Meya wa jiji hilo , wang'olewe.

“Waliungana na madiwani wa CCM na CUF kumpigia kura za kutokuwa na imani naye mheshimiwa Manyerere aliyekuwa Meya wetu, ni wasaliti hawafai, wamekiangusha chama, wanapaswa kuwajibishwa kama ulivyong’olewa uongozi wa wilaya hii.” Kilifafanua chanzo hicho.

Madiwani hao walitajwa kuwa ni Abukari Kapera(Nyamanoro), Hamis Kijuu (Mbugani), Adamu Chagulani (Igoma), Henry Matata (Kitangiri), Marietta Chenyenge (Ilemela), Lucy Kazungu na Upendo Robert, wote viti maalum.

Hoja nyingine iliyoibuliwa katika Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wapatao 94 na kuzua taflani iliyosababisha kutimuliwa uongozi wa wilaya hiyo ni pamoja na kutaka kujua kwanini Wabunge wake wana mamlaka makubwa kuliko viongozi wa Chadema wa wilaya na mkoa. KWA HABARI ZAIDI SOMA MZALENDO KESHO

This entry was posted in

Leave a Reply