Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE AMWAPISHA MTENDAJI MKUU NA MSAJILI WA MAHAKAMA

  Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Mtendaji mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili mkuu wa Mahakama na msajili wa mahakama ya rufani katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Walioapishwa leo ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga,Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana Ignus Paul Kitusi na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Panterine Muliisa Kente.Pichani Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga akila kiapo mbele ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) pamoja na maofisa waandamizi wa mahakama aliowaapisha leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam. (Wapili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga, (Wanne kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama, Ignus Paul Kitusi na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Panterine Muliisa Kente. (Picha na Freddy Maro).

This entry was posted in

Leave a Reply