* Yagoma kuomba raidhi, yasema tuhuma itazithibitisha mahakamani
* Yamtaka Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja
* Ni kwa kudai CCM inaingiza siala nchini.
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.
Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje ya nchi tena bila kulipia ushuru.
Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kweneye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam.
"Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti nimesema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala wasisubiri hizo siku saba", alisema Nape.
Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani badala ya kuomba radhi.
"Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama chao kinafutwa", alisema.
Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.
"Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini tena", alisema Nape.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
August
(57)
- ASENGA ASHINDA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA MKOA U...
- Makamu wa Rais Dkt Bilala ahutubia Mkutano mkuu wa...
- Aggrey Marealle agombea Ujumbe wa NEC ya CCM.
- Dkt. Mohammed Gharib Bilal Audhuria mkutano Iran.
- DC WA ZAMANI HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII D...
- CHADEMA WAPATA PIGO MAKETE
- BHAA ACHUKUA FOMU ZA UWAKILISHI JIMBO LA BUBUBU.
- CCM YAIKOMALIZA CHADEMA
- DEREVA ACHUKUA FOMU KUMU KUMVAA MABINA UENYEKITI W...
- RAIS KIKWETE NA FAMILIA YAKE WAHESABIWA KATIKA SEN...
- CHADEMA YAKOSA MVUTO MOROGORO
- DIWANI KATA YA KWADELO AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA
- RAIS KIKWETE AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO
- MPANGO WA KASI YA UWEZESHAJI WA WANAWAKE WAZINDULI...
- ABDALLAH BULEMBO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI JUMUIYA...
- CCM YAMTEUA NDG HUSSEIN I. MAKUNGU KUGOMBEA BUBUBU.
- DR MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA B...
- HARAKATI ZA UCHAGUZI WA CCM WILAYA NA MKOA WA LIND...
- UMOJA WA VIJANA (UVCCM) WILAYA YA LINDI MJINI WAFA...
- CCM KUKATA RUFANI KUTENGULIWA USHINDI WA MBUNGE WA...
- CCM ARUSHA WAKAMILISHA UCHAGUZI KWA ASILIMIA 90
- CCM YAMSHUKIA DK. SLAA, YAKANUSHA KUINGIZA SILAHA ...
- Tonight - Filamu Lounge presents LUMUMBA at Nafasi...
- MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI WASUSIE ZOEZI LA ...
- MWILI WA MPIGANAJI ALFRED MBOGORA WASAFIRISHWA LEO
- EID MUBARAK
- CHADEMA MWANZA SASA WATISHANA KUNG'OANA
- MAJINA YA WAGOMBEA UVCCM "UPDATED"
- KIJANA WA CHAMA ABUBAKAR ASENGA AMTEMBELEA MZEE KI...
- NAPE AFUTURISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI MOROGORO
- JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MWANAFUNZI, BUNDA
- HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,...
- KIBONZO
- WAZIRI MKUU PINDA ATOA CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI KU...
- MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA CHANJO
- Baraza la Vijana Dodoma
- CHADEMA WALIVYOUMBUKA UINGEREZA
- ONYESHO LA PICHA ZA MWANZO MILINGA LAFANA MJINI DAR
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZIMBABWE
- RAIS KIKWETE AMWAPISHA MTENDAJI MKUU NA MSAJILI WA...
- BALOZI MAHALU ASHINDA KESI
- MATUKIO YA ZIARA YA UJUMBE WA NGAZI YA JUU YA CCM...
- RAIS AREJEA NCHI BAADA YA KUMALIZA MKUTANO WA NCHI...
- ORODHA YA WALIOCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI MBAL...
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAON...
- RAIS KIKWETE AMEWASILI SALAMA MJINI KAMPALA, UGAND...
- Dk.SHEIN AZINDUA MASHINE YA KUNIA MPUNGA
- RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA K...
- UVCCM 'WAKANYAGANA' KURUDISHA FOMU LEO
- PINK CARAVAN NDANI YA DAR
- CCM DMV WAFUTURISHA
- FOMU ZAANZA KUCHUKULIWA UVCCM
- NGASSA RASMI SIMBA, AKABIDHIWA JEZI NO 16 LEO
- WANAFUNZI 94 WA MT.EVEREST WAPATA KIPAIMARA
- UFUNGUZI WA TAWI LA CCM WASHINGTON, DMV.
- HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA...
-
▼
August
(57)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.