|
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mjini Mheshimiwa Dr Nassor Hamid akihutubia hadhira ya wajumbe ambao wapiga kura katika uchaguzi huo wa Wilaya yake uliofanyika Katika Ukumbi wa Hotel ya Lindi Oceanic. |
Katika mchakato ambao unaendelea kote nchini ambapo Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake zimekuwa zinaendelea nao wa Uchaguzi wa Viongozi wake katika hatua na nyadhifa mbalimbali, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Lindi mjini, wmefanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo katika wilaya yao,pia wamefanya uchaguzi wa wajumbe wengine wa halmashauri kuu ya Wilaya na mkutano mkuu wa Wilaya.
Uchaguzi huo ambao umefanyika katika Ukumbi wa Lindi Oceanic Hotel umefunguliwa na mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mjini Mheshimiwa Dr. Nassor Ally Hamid, lakini pia ulihudhuriwa na wageni mbalimbali ambao ni viongozi na wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa kutoka katika kila Kata y Wilayani humo, ambapo takribani wajumbe 300 kutoka kata 18 walihudhuria na kupiga kura katika uchaguzi huo.
|
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Lindi Mjini (UVCCM) Ndugu Juma Seif Bahatimbaya (kushoto) na Ndugu Said Rashid Namponda.(kulia)
|
|
wajumbe mbalimbali kutoka katika kata 18 za wilaya ya Lindi Mjini waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Mkoa ambao unachagua viongozi mbalimbali wa jumuiya ngazi hiyo ya wilaya.
|
|
Wajumbe mbalimbali waliojitokeza katika Mkutano huo. |