Google PlusRSS FeedEmail

MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI WASUSIE ZOEZI LA SENSA TANGA

 TANGA, TANZANIA
Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korogwe, Tanga, Juma Salehe (52) amekamatwa na polisi akihamasisha mitaani kwa kipaza sauti wananchi walikatae zoezi hilo.

Habari zilizofikia meza ya  CCM Blog,  zimesema mratibu huyo wa elimu ambaye anadaiwa kuwa pia ni Sheikhe wa Msikiti wa Mazinde katika kata hiyo ya Vugiri anashikiliwa katika kituo cha mamlaka mji mdogo wa Mombo uliopo wilani ya Korogwe vijijini mkaoni Tanga.

Imeelezwa amekamatwa jana saa 8.00 mchana ndani ya msikiti wa Mazinde, kutokana na  wananchi kutoa taarifa dhidi ya mtu huyo kuendesha vitendo ambavyo vilikuwa vikiwachanganya wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa.

"Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya shitaka lake", amesema Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Coastantin Massawe.

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Naudhika sana na tabia hii ya kutoshindanisha hoja. Kwanini mtu au watu wakiwa na jambo lao wasisikilizwe? hii kupuzana siyo tabia nzuri maana watu fulani wana weza kufikiri wanaonewa.Hili la ndg zetu waislam kutohesabiwa ni la msingi sana kwani wana sababu kwa maoni yangu ila majibu yaliyorolewa ni shallow sana sasa wakigoma mtapataje takwimu sahihi?

Leave a Reply