Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimepata aibu ya mwaka hapa jijini London baada ya Watanzania kususa kuhudhuria mkutano wao waliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.
Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa.
Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.
Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.
Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.
Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema…. “Gwanda linanuka RUSHWA meku”….huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.
Katika mahudhurio hayo machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “…jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja…wanafikiri hapa ni walipotoka..ovyoo.”
Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata wachama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.
Habari hii imeandikwa na Rukia Kilemile ambaye ni mwandishi wa Kujitegemea anayepatikana kwa email
rkilemile@gmail.com. Mwandishi huyu ni mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United Kingdom.
Mwandishi si mwana chama wa chama chochote cha siasa.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
August
(57)
- ASENGA ASHINDA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA MKOA U...
- Makamu wa Rais Dkt Bilala ahutubia Mkutano mkuu wa...
- Aggrey Marealle agombea Ujumbe wa NEC ya CCM.
- Dkt. Mohammed Gharib Bilal Audhuria mkutano Iran.
- DC WA ZAMANI HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII D...
- CHADEMA WAPATA PIGO MAKETE
- BHAA ACHUKUA FOMU ZA UWAKILISHI JIMBO LA BUBUBU.
- CCM YAIKOMALIZA CHADEMA
- DEREVA ACHUKUA FOMU KUMU KUMVAA MABINA UENYEKITI W...
- RAIS KIKWETE NA FAMILIA YAKE WAHESABIWA KATIKA SEN...
- CHADEMA YAKOSA MVUTO MOROGORO
- DIWANI KATA YA KWADELO AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA
- RAIS KIKWETE AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO
- MPANGO WA KASI YA UWEZESHAJI WA WANAWAKE WAZINDULI...
- ABDALLAH BULEMBO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI JUMUIYA...
- CCM YAMTEUA NDG HUSSEIN I. MAKUNGU KUGOMBEA BUBUBU.
- DR MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA B...
- HARAKATI ZA UCHAGUZI WA CCM WILAYA NA MKOA WA LIND...
- UMOJA WA VIJANA (UVCCM) WILAYA YA LINDI MJINI WAFA...
- CCM KUKATA RUFANI KUTENGULIWA USHINDI WA MBUNGE WA...
- CCM ARUSHA WAKAMILISHA UCHAGUZI KWA ASILIMIA 90
- CCM YAMSHUKIA DK. SLAA, YAKANUSHA KUINGIZA SILAHA ...
- Tonight - Filamu Lounge presents LUMUMBA at Nafasi...
- MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI WASUSIE ZOEZI LA ...
- MWILI WA MPIGANAJI ALFRED MBOGORA WASAFIRISHWA LEO
- EID MUBARAK
- CHADEMA MWANZA SASA WATISHANA KUNG'OANA
- MAJINA YA WAGOMBEA UVCCM "UPDATED"
- KIJANA WA CHAMA ABUBAKAR ASENGA AMTEMBELEA MZEE KI...
- NAPE AFUTURISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI MOROGORO
- JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MWANAFUNZI, BUNDA
- HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,...
- KIBONZO
- WAZIRI MKUU PINDA ATOA CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI KU...
- MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA CHANJO
- Baraza la Vijana Dodoma
- CHADEMA WALIVYOUMBUKA UINGEREZA
- ONYESHO LA PICHA ZA MWANZO MILINGA LAFANA MJINI DAR
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZIMBABWE
- RAIS KIKWETE AMWAPISHA MTENDAJI MKUU NA MSAJILI WA...
- BALOZI MAHALU ASHINDA KESI
- MATUKIO YA ZIARA YA UJUMBE WA NGAZI YA JUU YA CCM...
- RAIS AREJEA NCHI BAADA YA KUMALIZA MKUTANO WA NCHI...
- ORODHA YA WALIOCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI MBAL...
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAON...
- RAIS KIKWETE AMEWASILI SALAMA MJINI KAMPALA, UGAND...
- Dk.SHEIN AZINDUA MASHINE YA KUNIA MPUNGA
- RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA K...
- UVCCM 'WAKANYAGANA' KURUDISHA FOMU LEO
- PINK CARAVAN NDANI YA DAR
- CCM DMV WAFUTURISHA
- FOMU ZAANZA KUCHUKULIWA UVCCM
- NGASSA RASMI SIMBA, AKABIDHIWA JEZI NO 16 LEO
- WANAFUNZI 94 WA MT.EVEREST WAPATA KIPAIMARA
- UFUNGUZI WA TAWI LA CCM WASHINGTON, DMV.
- HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA...
-
▼
August
(57)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.