Google PlusRSS FeedEmail

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) UWANJA WA JAMHURI, DODOMA, 15 AGOSTI 2012.



Mhe. Spika;
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
 Mhe. Steven Wassira, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Uratibu na Mahusiano,;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mhe. Daktari Rehema Nchimbi, Mheshimiwa Steven Wassira (Mb);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;,
Mheshimiwa Dr. Rehema Nchimbi;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia: Tanzania, Uganda na Burundi,
Bwana Philippe Dongier;
Ndugu Peniel Lyimo, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa TASAF;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia;
Wawakilishi wa Ndugu Peniel Lyimo;
wWashirika  wetu wangine wa mMaendeleo; ,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nawa  Serikali;
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF;
Wageni wWaalikwa;
Mabibi na Mabwana:;:

Shukrani
Ndugu Wananchi:
Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Steven Wassira na Nndugu Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Kamati yake kwa kunialika nije kushiriki nanyi kwenye uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya TASAF.Tarehe 30 Machi 2000 tulizindua Awamu ya Kwanza ya Mfuko wa Kwa kuwa huko tulipotoka tumepata mafanikio ya kutia moyo, naomba nianze kwa kutoa pongezi na kuwashukuru wote walioshiriki kufanikisha utekelezaji wa awamu mbili za TASAF zilizotangulia. 
Pongezi
Ndugu Wananchi;     
Napenda kuishukuru kwa dhati Benki ya Dunia na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo wa wao hapa nchini kwa kushirikiana na sisi kutekeleza miradi mbalimbali ya TASAF tangu mwaka 2000. Siku zote  Benki ya Dunia imekuwa mwenzetu muhimu na wa kutumainiwa na hii  inasikiliza hoja zetu na kuzingatia vipaumbele vya sSerikali na wananchi wa Tanzania yetu katika jitihada zetu za kupambana na umaskini na kujiletea maendeleo.  Tunafurahishwa sana na sera ya kusikiliza vipaumbele vyetu.  Jambo hilo Hali hii ndiylo limetuwezesha sisi kushirikiana nao kubuni mpango huu wa TASAF unaofadhiliwa na ubia mzuri wa maendeleo kati yetu Serikali na Benki ya Dunia, , kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, Serikali zetu mbili na wananchi wa nchi yetu. 
Natoa ipongezai nyingi kwa sana Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, chini ya uenyekiti imara wa Ndugu Peniel Lyimo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa uongozi wake thabiti wa kusimamia vizuri shughuli za TASAF.  Aidha, nampongeza Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa usimamizi wake thabiti.  Hali kadhalika  nNawapongeza pia viongozi na watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara , Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kazi nzuri waifanyayo ya usimamizi na utekelezaji wa miradi katika awamu iliyotangulia. Bila uongozi wao thabiti, mafanikio ya Awamu zya Kwanza na Pili yangekuwa ni ndoto. Kwa namna ya pekee nawapongeza wananchi wote walioitikia wito na kuchangia kwa hali na mali kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe.

INAENDELEA...!

This entry was posted in

Leave a Reply