TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI WA MGOMBEA BUBUBU
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyofanya kikao chake leo tarehe 24/8/2012 imemteua Ndg. Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) kuwa mgombea wa kiti cha uwakilishi kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Bububu.
Aidha, Kamati Kuu imemteua Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzindua kampeni hizo na Mhe. Balozi Seif Alli Iddi, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufunga kampeni hizo.
Pia, Kamati Kuu imemteua Mhe. Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kuongoza kampeni hiyo. Kamati Kuu imewataka wanachama na wapenzi wa Chama kwenye jimbo la Bububu kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha Chama kinashinda kwenye uchaguzi huo.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
24/08/2012